Waziri
mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameelezea mshangao wake binafsi kwa
mwanajeshi wa Israeli wa asili ya Ethiopia ambaye alipigwa na polisi wa
Israeli hali iliyosababisha kutokea kwa maandamano.
Bwana Netanyahu alimuambia Damas Fikadeh kuwa kitendo hicho hakikubaliki, na madabiliko yanahitaji kufanywa. Israel
Bwana Fikadeh alisema alitiwa
moyo na matamshi yake waziri mkuu na ni wakati wa kumaliza ghasia za
ubaguzi dhidi ya Waisraeli wa asili ya Ethiopia. Wakati wa ghasi hizo za siku ya jumamosi usiku mjini Tel Aviv takriban watu 50 walijeruhiwa. Waandamanaji Israel
Wakati huohuo rais wa Israeli
Reuven Rivlin amesema kuwa ni makosa jinsi Israeli inavyowafanyia
wayahudi wenye asili ya Ethiopia.
Akizungumza baada ya maandamano
yenye ghasia mjini Tel Aviv bwana Rivlin alisema kuwa kidonda kilicho
wazi kimeonekana nchini Israeli , lakini ghasia sio suluhu.
No comments:
Post a Comment