Katika maeneo mengi jana, wanafunzi pamoja na
abiria walikaa vituoni kwa muda mrefu, ingawa baadhi ya magari binafsi
yalikuwa yanatoa msaada kwa baadhi yao.
Mkazi wa Songea, Nasri Isack alisema watoto wake
walishindwa kuhudhuria masomo na alilazimika kukodi teksi ili mwanaye
awahi shuleni kufanya mtihani wa kidato cha sita.


Aliongeza kuwa yeye binafsi alilazimika kukodi teksi kwenda hospitali ya Peramiho kwenye matibabu baada ya daladala kugoma.
“Hivi kwanini Serikali haitaki kumaliza hili tatizo, wanapata furaha gani kuona wananchi tunavyoteseka na huu mgomo usioisha?
“Leo nimetoa zaidi ya Sh60,000 ili kumwahisha
mwanangu akafanye mtihani wa kidato cha sita, pamoja na mimi mwenyewe
kwenda kutibiwa Peramiho, hii ni pesa nyingi kwangu kwani kusingekuwa na
mgomo tungetumia Sh3,000 tu, nimesikitika sana,” alisema.
Jijini Mbeya makundi ya wanafunzi wakiwamo wa
kidato cha sita walianza kusota barabara tangu saa 11.30 alfajiri ambapo
daladala hazikuonekana ingawa bajaji na pikipiki zilikuwa zikifanya
kazi wakati huo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Sangu, Andongwisye
Bukuku aliliambia gazeti hili kwamba baadhi ya wanafunzi wake hususani
wa kidato cha sita walioanza mitihani yao ya mwisho waliathirika na
mgomo huo.
No comments:
Post a Comment