MSHAMBULIAJI wa Yanga, Simon Msuva amerejea nchini akitokea
Afrika Kusini alikokwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, lakini
machale yameicheza klabu yake.
Wameshtukia kwamba inawezekana kuna dili Simba
inacheza chinichini ili Yanga imwachie aende Sauzi halafu msimu ujao
atue Msimbazi.
Unajua Yanga walichofanya? Wamembananisha Msuva.
Vigogo wa Yanga wameiagiza sekretarieti yake kuwa makini na kuweka
vipengele vya kumbana Msuva kama dili lake na klabu hiyo ya Afrika
Kusini litatiki.
Wataweka vipengele muhimu viwili katika mkataba wake na klabu hiyo huku kimoja kikiwekwa maalumu kuikomoa Simba.

Msimbazi wanamhitaji Msuva kwa muda mrefu ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Wekundu hao Zacharia Hans Poppe amekuwa akitoa kauli mbalimbali juu ya kiungo huyo wanayemmezea mate.
Kipengele ambacho Yanga imetaka kiwemo katika
mkataba wake na Bidvest Wits inayonolewa na beki wa kulia wa zamani wa
Afrika Kusini ‘Bafanabafana’ Gavin Hunt ni kutoa sharti moja kwamba
endapo Msuva ataamua kurudi nchini mara baada ya kuachana na klabu hiyo
moja kwa moja asisaini Simba bali arudi Yanga.
Akili ya Yanga katika kipengele hicho ni kutaka
kuhakikisha Msuva havai jezi ya Simba. Yanga wanahisi kwamba inaweza
kuwa janja ya Simba kumpeleka Msuva Sauzi ili wamrudishe kirahisi
Msimbazi kuwakomoa Yanga ambao kwa sasa wanaitambia Simba mtaani haswa
kutokana na makali ya Amissi
Tambwe.
Tambwe.
Kipengele cha pili ambacho Yanga itakiweka ni
kutaka kuhakikisha inanufaika na mauzo yoyote yatakayofanywa na Wits kwa
Msuva kuuzwa kwenye klabu nyingine.
“Unajua hili suala la Msuva kwenda huko limekuja
wakati ambao hapa kati Simba wameongea mengi sana kwamba watamsajili
Msuva, sasa tumeamua kujiweka katika maeneo salama na uwepo wa kipengele
hicho cha kwanza nilichokutajia ni wazi Simba watasubiri kwanza ili
tumkatae Msuva ili wampate wakati huo akirudi,” alisema.
Wits yafunguliwa mashtaka.
Yanga inataka kuishtaki Wits kwa kitendo cha
kumfanyia majaribio Msuva bila ya kupewa idhini na klabu hiyo.
Yanga bado ina mkataba na Msuva utaofikia tamati mwishonmi mwa msimu wa 2015/2016 ambapo katika malalamiko yao wanataka CAF (shirikisho la soka la Afrika) kuchunguza uhalali wa Wits kumfanyia majaribio mchezaji mwenye mkataba.
Yanga bado ina mkataba na Msuva utaofikia tamati mwishonmi mwa msimu wa 2015/2016 ambapo katika malalamiko yao wanataka CAF (shirikisho la soka la Afrika) kuchunguza uhalali wa Wits kumfanyia majaribio mchezaji mwenye mkataba.
No comments:
Post a Comment