Wednesday, 1 April 2015

CHELSEA YAMWINDA THEO WALCOT ...

             
 
Kilabu ya Chelsea inaiangazia kwa karibu hali ya kandarasi ya mchezaji wa Chelsea Theo walcot katika kilabu ya Arsenal na huenda ikamsajili iwapo atakuwa huru mwishoni mwa msimu huu.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza atakuwa amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake na hadi kufikia sasa hajapewa mkataba mpya na Arsenal.

Chelsea walianza kumfuatilia Walcot aliposalia na miezi 12 ya kandarasi yake miaka mitatu iliopita kabla ya kutia sahihi mkataba mpya katika uga wa Emirates

UCHAGUZI WA NIGERIA FUNZO KWA TANZANIA ..>>

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wananchi wa Nigeria walipiga kura kumchagua Rais katika uchaguzi wenye ushindani mkali kati ya Rais wa sasa, Goodluck Jonathan na mpinzani wake Jenerali Muhamadu Buhari.

Katika makala haya, mtangazaji na mwandaaji wa vipindi katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Salimu Kikeke anazungumzia uzoefu alioupata katika mchakato wa uchaguzi huo, kama alivyohojiwa na mwandishi wetu.

Swali: Tueleze uzoefu wako kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kuandikisha wapigakura na pengine changamoto zake ulizozibaini nchini Nigeria?

Jibu: Nadhani dunia inaelekea katika mfumo wa kidijitali na itafika wakati pengine kila nchi duniani itakuwa ikitumia mfumo wa kielektroniki, katika uchaguzi, lakini pia katika mambo mengine mbalimbali.

Kwa kuwa bado ni mfumo mpya, watu wengi hawajaweza kuelewa hasa unafanyaje kazi. Nadhani uzuri wa mfumo huu, ni kwamba una uwazi zaidi na matokeo yake yanaweza kuaminiwa na wapiga kura kwa kuwa ni mashine ambazo hufanya kazi na hilo pia hupunguza uwezekano wa makosa ambayo huweza kufanywa na binadamu.

Vifaa vya kusomea kadi (card readers) vina betri yenye uwezo wa kufanya kazi kwa saa 14, na husoma kadi moja kwa chini ya sekunde 60 na ni vigumu ‘kuchakachua’ labda mtu aghushi ‘VIN,’ yaani namba maalumu ya mpigakura.

Kwa hiyo mfumo huu una ufanisi mkubwa, lakini kama teknolojia nyingine zozote mpya, zina changamoto zake siku za mwanzo, na zinapozoeleka hali inakuwa tofauti.

Swali: Kipi kimekukosha na kukusononesha kuhusu mchakato mzima wa uandikishaji na uendeshwaji wa kampeni nchini Nigeria?

Jibu: Hii ni moja ya nchi zinazoelezwa kuwa na demokrasia kubwa barani Afrika. Pia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mingi, uchaguzi huu una ushindani mkali kati ya wagombea urais ambao ni Goodluck Jonathan wa chama tawala PDP na Jenerali Muhhamadu Buhari wa chama cha upinzani APC, wanavutana vikali kabisa.

Kitu ambacho kimenivutia hasa ninapozungumza na wananchi wa hapa, ni kutaja suala la amani. Licha ya vuta nikuvute iliyopo, wengi wanasema cha msingi ni kufanya uchaguzi huu kwa amani. Kumekuwa na vijembe vya hapa na pale, na wakati mwingine ghadhabu ambazo unaweza kudhani zitavuka mipaka na kuleta tafrani, lakini hilo halijajitokeza kwa kiwango kikubwa cha kutisha- ukiacha matukio ya Desemba mwaka jana, ambapo kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya haki za Binadamu watu takriban 58 waliuawa katika ghasia zinazihusiana na uchaguzi katika sehemu mbalimbali.

Pamoja na kuwa masuala makuu kama usalama, ufisadi na uchumi ni mambo yanayozungumzwa zaidi kwenye vyombo vya habari, wananchi wengi wa kawaida wanataka mambo ya kila siku maishani kama vile umeme na maji, lakini kubwa kuliko yote wanataka amani.

Kampeni kwa jumla zimekuwa salama na kwa kuwa kuna ushindani mkali katika urais, wagombea wamekuwa wakijinadi kwa kusema kinagaubaga jinsi watakavyokabiliana na changamoto za taifa hili. Jambo zuri pengine ni kuwa wote wamewahi kuongoza taifa hili.

PAPA DENIS ASIFU MTANDAO WA J Z ..>>

Dennis Mwangi ama Papa Denis ni msanii wa injili nchini Kenya.
Baadhi ya majina makubwa katika fani ya burudani wamezindua upya huduma ya usajili wa miziki yao - Tidal,ambapo wanatoza malipo kadri msanii anavyotoa muziki ama video .

Huko Newyork New York, Madonna, Rihanna, Beyonce and Alicia Keys walikua miongoni mwa wanamuziki waliotangaza kuwa watashirikiana umiliki katika Tidal,
ambayo ilianza kuchezwa mwezi oktoba mwaka jana na pia kununuliwa na nyota wengine wa muziki Jay Z.

Tidal ni mshindani wa moja kwa moja wa Spotify, ambayo huwapatia watumiaji huduma kama hiyo.
Dennis Mwangi ama Papa Denis ni msanii wa injili nchini Kenya.

Anaelezea jinsi mtandao waTidal unavyoweza kuwasaidia wasanii kuuza muziki wao tofauti na hali ilivyo kwa wasanii Kenya

KIJANA WA KICHINA HENRY CHAU ALIECHINJA FAMILIA YAKE NA KUWALA .. HUYU HAPA ..

Mwanamume mmoja raia wa Hong Kong amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji,kutawanya viungo vya nduguze ,kuwanyunyizia chumvi na kuwapika.
Mtuhumiwa huyo wa mauaji ya kushangaza ana umri wa miaka thelathini na mmoja jina lake ni Henry Chau aliibua hisia za walio wengi katika kesi ya namna yake mnamo 2013 wakati kichwa cha mamake mkubwa pamoja na babake vilipobainika kuhifadhiwa katika majokofu mawili tofauti.
Majaji wa mahakama kuu nchini Hong Kong ,wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelea walisikiliza namna Chau alivyotekeleza mauaji yake ,kwanza huua, pili hutawanya viungo vya maiti na kisha huwanyunyizia chumvi ili kuongeza ladha ,na anasema yote hayo ni matokeo ya mapenzi yake kwa nyama choma ya kiti moto,na nyama hiyo ya binaadamu zikisha iva ama kuchomwa huwa anafunga nyama hizo katika makasha ya chakula paoja na ubwabwa,na polisi walipofanya upekuzi katika nyuma yake walikuta baadhi ya viungo katika chombo cha kuhifadhia taka.
Akitoa hukumu dhidi ya kesi hiyo,jaji Michael Stuart-Moore alimuelezea Chau kama mbinafsi mwenye msongo wa mawazo kutokana na mafanikio mabaya yake ya maisha na asiye na huruma kwa wengine.
Chau, alihukumiwa adhabu mara mbili kifungo cha maisha jela na miaka tisa namiezi minne kwa makosa mawili tofauti kwa kuvunja sheria ya kuzika miili ya familia yake isivyo kawaida kosa ambalo alikiri baadaye.
Rafiki wa Chau anayehusishwa katika mauaji hayo alikutwa hana hatia mwishoni mwa wiki iliyopita .
Taarifa za kupotea kwa wanafamilia wa Chau zilipoibuliwa ,Chau alidanganya kuwa jamaa zake walikwenda China,lakini baadaye alijisahau na kumuandikia rafikiye kupitia ujumbe mfupi wa simu kwamba aliwaua jamaa zake.
Chau mwenyewe hujiita mwendawazimu katika ujumbe aliokuwa akiwatumia watu wake wa karibu na kusema kwamba hawezi kumuonea huruma mtu yeyote kutokana na maumivu aliyopitia wakati wa makuzi yake utotoni mpaka anakuwa mtu mzima.
Na alimua kuwadanganya polisi ilia pate wasaa wa kuwaaga marafiki zake.

WAJUMBE WATOFAUTIANA KUHUSU IRAN ..

Wajumbe wa mazungumzo ya mpango nyuklia wa Iran wanaokutana nchini Switzerland wametofautiana misimamo yake katika mkutano ulioendelea hadi usiku wa leo.
Wakati Waziri Mkuu wa Urusi Sergei Lavrov, akisema mazungumzo hayo yamefikia maamuzi katika mambo yote ya msingi kuhusiana na suala la Iran,Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif yeyeanasema alitaraji kuwa wangeanza kuanda rasmu ya mapendekezo. 
Lakini ujumbe kutoka nchini Marekani unasema kuwa si mambo yote ya msingi kuhusiana na mpango wa Iran yameorodheshwa katika mkutano,wakati waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius akidai kuwa analazimika kuondoka mkutanoni hapo kuwahi mkutano mwingine mjini Paris.

CCM NA CUF HUKO ZNZ WAZIPIGA ZA JUU JUU .. aka Matumla..

UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM) umelaani na kusikitishwa na kauli za viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kuitupia lawama CCM kwa kudai imehusika katika kushambuliwa wafuasi wao.
Wakati CCM wakitoa kauli hiyo, CUF kimemtupia lawama Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Balozi Seif Ali Idd kuwa ndiye amekuwa akitoa kauli za kuchochea vurugu visiwani humo.
Taarifa ya UVCCM Zanzibar kulaani matamshi hayo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari na Naibu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka.
Wafuasi wa CUF walivamiwa na kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa CCM, ambapo katika vurugu hizo watu 25 waliokuwa wakitokea katika mkutano uliokuwa unafanyika Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja walijeruhiwa.
Shaka alisema katika taarifa yake kwamba baadhi ya viongozi wa CUF wakiwamo wawakilishi wa chama hicho, kwa nyakati tofauti wamesikika na kunukuliwa na vyombo vya habari wakidai shambulio hilo la kudhuru limepangwa na kufanywa na vijana wa CCM jambo alilosema si kweli na halina ushahidi.

“Shutuma za CUF kwa namna moja au nyingine zimejiegemeza katika kuficha ukweli wa chanzo halisi kwani itakumbukwa hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad katika moja ya mikutano yake ya hadhara alioufanya Kiembesamaki, sehemu kubwa ya hotuba yake ililenga kuwahamasisha na kuwachochea vijana wa chama chake kujiandaa kwa vurugu na kutotii sheria za nchi.
“UVCCM tunaamini vitendo hivyo viovu na vya kikatili vilivyofanyika ni matokeo ya matamshi ya uchochezi yaliyotolewa na katibu mkuu huyo na kuonyesha ni chimbuko la kuanza kushamiri matukio ya uvunjaji wa sheria kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu,” alisema.

Alisema mara kadhaa UVCCM imekuwa ikihimiza na kuwataka viongozi wa juu wa kisiasa kuchunga ndimi zao ili kuendesha siasa za kuvumiliana, kushindana kwa nguvu ya hoja, pia kuyaenzi na kuyalinda maridhiano ya kisasa yaliyofikiwa kati ya vyama vya CCM na CUF hadi kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010.
“Inashangaza hivi leo kumuona mmoja kati ya viongozi wanaojinasibu ni muumini na waasisi wa maridhiano akipanda majukwaani na kuanza kurejesha siasa za “mti kwa macho” na kushupaliana huku akitoa semi za uvunjaji wa sheria, akisema yuko tayari hata kupigwa mabomu na kuwa wa kwanza kuuawa hali inayoonyesha anakumbatia uvunjaji wa sheria,” alisema Shaka katika taarifa yake.


KAULI YA CUF
Chama cha CUF kimesema kutokea kwa vurugu kisiwani Unguja juzi, kumesababishwa na kauli iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd.


Akizungumza na MTANZANIA jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Salum Bimani, alisema dalili za kutokea kwa vurugu na watu kujeruhiwa zilianza muda mrefu.

“Leo limetokea hili, Balozi Seif Ali Idd ameshindwa hata kulaani, jambo kubwa amekuwa akilitengeneza kwa kauli zake, mara utamsikia akisema Serikali haitolewi kwa makaratasi na eti watashughulikia CUF.
“Si hilo tu, lakini wapi ulisikia mkutano wa CUF tumefanya vurugu, ila ni mikutano ya CCM tu, kwa hali hiyo tunamtaka Rais Dk. Shein aliangalie hili na achukue hatua dhidi ya watu wote wanaotoa lugha za kichochezi,” alisema Bimani.


GENERAL MAHAMMUD RAIS MPYA WA NIGERIA ... !!