Wednesday, 3 June 2015

NGUVU ISIYOZUILIKA ....>>

Mambo Vipi Rafiki wa LOWASSA na mkataa UMASIKINI .... UNAEPENDA ELIMU .
Naendelea kufuatilia kwa ukaribu mbio za kuelekea uchaguzi mkuu 15'' mwaka huu mwezi wa kumi kama ilivyosisitizwa na Mh. Rais wa jamhuri ya muungano Dkt. J. M . K
Maneno ni mengi sana toka kwa watangaza NIA yamesemwa , wengine jazba za wazi wazi zinawapanda na wanasahau kua hatupo vitani hii ni siasa , wanasema kwa ukali wenye hasira ya CHUKI , Hii sio sawa .
Wengi wamenyoosha kidole kwa KINARA WAO mzee LOWASSA .. Japo hawasemi moja kwa moja ila wanafumba kwa kusema LOWASSA anatawanya fedha na kuwalipa watu wamuunge mkono na kumshabikia ...
Mimi sio msemaji wa LOWASSA na sina position ya kusema kwa hakika juu ya LOWASSA na mwenendo wake wa kila siku .. ila kama shabiki wa LOWASSA wa damu na mtanzania ninaependa maendeleo na kiongozi anaeona mbali .. ninaweza kua shahidi wa kwanza wa LOWASSA KAMA UTASIMAMA NA KUSEMA ANATUPA PESA ...
Marafiki zangu wa karibu wanakua mashaidi wa pili wa LOWASSA dhidi ya kauli hii ya kipuuuzi ya kwamba tunalipwa kumpaisha LOWASSA ....
Haiumizi kichwa ila ni vyema habari ikaeleweka .. tumepaki magari yetu kwa kumuunga mkono lowassa tunatumia pesa za mfukoni kwetu , tunalipa watu wa kutusaidia kufanya maswala ya kitaalam ambayo ni lazima yafanyike kwa utaalam .. LOWASSA hajui ... Wala hana habari kua kuna mitkasi mikubwa inaendelea kwa niaba yake.... ni LOVE tu mzee ni mapenzi tu kwa huyu mzee .
Sasa SIRI NI NINI hata tumpende LOWASSA kiasi hiki ?
Sitamumunya maneno .. SIRI NI KUCHOKA ... Tumechoka kinoooma na haya mambo ya sasa .. mmetunyanga'nya dili zetu kwakua mtoto wa prezda , tunawapa mikopo hamlipi mnasingizia kazi zikitoka mtatupa tukatane juu kwa juu , haya sawa miaka sasa imepita pesa hamlipi kazi hamtoi .. tukidai hela zetu mnatutishia mtatupoteza kwakua kaya ni ya yenu ... dooohhh ! kweli ?
Alafu anatokea LOWASSA nae anawalilia kama sisi .. kwanini tusimuunge mkono tukamaliza huku kujuana juana kunakotuulia TAIFA .
Kwa sasa haijalishi unajua NINI ... Iaangaliwa unamjua NANI ? halafu mnasema nchi ni yetu sote kweelii? Hii mnasema ni nchi yetu sote ... huu si utoto kwa mtu MZIMA ?
Angalia kazi ya LOWASSA MPAKA SASA . >>>


LOWASSA
As received ... Plz sambaza kwa marafiki ujumbe huu wenye matumaini tukiwa safarini rafiki wewe wa LOWASSA ...
🔝Ikiwa mchakato wa kuchukua fomu unaedelea, ebu tutumie dakika chache kutafakari nguvu ya kila mgombea... Nguvu ya mgombea au mgombea mtarajiwa tunaweza kuijua kutokana na jinsi anavyoungwa mkono na wananchi, wanachama, wajumbe wa vikao mbalimbali, na viongozi kwa ujumla wao...
Mpaka sasa ni takriban wagombea 9 washatangaza nia, ebu sasa tuangalie idadi ya viongozi/wajumbe waliowasindikiza siku wanatangaza nia (Hasa Wenyeviti wa CCM Mikoa, WaNec, wabunge na wajumbe wa mkutano mkuu)....
1. Edward Lowassa.. Waliohudhuria
. Wenyeviti wa Mikoa~23 kati ya Mikoa 30
. Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC)~286 kati ya 378
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa~1967/2600's..
. Wabunge wa JMT~168/357
2. Fredrick Sumaye.. Waliohudhuria
. Wenyeviti wa Mikoa~0
. Wajumbe wa Halmashauri kuu (NEC)~0
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa~2
. Wabunge~0
3. Prof. Mack Mwandosya.. Waliohudhuria
. Wenyeviti wa Mikoa~0
. Wajumbe wa NEC~2
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu~4
. Wabunge~2
4. Mwigullu Nchemba.. Waliohudhuria
. Wenyeviti wa Mikoa~0
. Wajumbe wa NEC~3
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu~7
. Wabunge~4
5. Stephene Wassira.. Waliohudhuria
. Wenyeviti wa Mikoa~0
. Wajumbe wa NEC~3
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu~7
. Wabunge~3
6. Dr. Titus Kamani.. Waliohudhuria..
. Wenyeviti wa Mikoa~1
. Wajumbe wa NEC~2
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu~3
. Wabunge~1
7. Prof. Muhongo... Waliohudhuria
. Wenyeviti wa Mikoa~0
. Wajumbe wa NEC~0
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu~2
. Wabunge~1
8. Makongoro Nyerere.. Waliohudhuria..
. Wenyeviti wa Mikoa~0
. Wajumbe wa NEC~1
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu~3
. Wabunge~2
9. Balozi Karume.. Waliohudhuria
. Wenyeviti wa Mikoa~0
. Wajumbe wa NEC~0
. Wajumbe wa Mkutano Mkuu~2
. Wabunge~0
Mytake:... Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.... Hii ndiyo safari ya Matumaini.........
🔝 www.tutokevipi.blogspot.com
Instagram - tweeter
Tutokevipi?

Tuesday, 2 June 2015

F.B.I KUMCHUNGUZA BLATA ....!

 
BLATA
Imeripotiwa kuwa Raisi wa Fifa,Sepp Blatter anafanyiwa uchunguzi na maafisa wa marekani ili kuthibitisha tuhuma za rushwa zinazomkabili vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.
Taarifa hiyo inakuja baada ya Blatter kutangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake.

Wakati ambao waendesha mashtaka nchini Marekani wanaoifuatilia tuhuma za rushwa walikamata maafisa saba wa Fifa nchini Switzerland kati ya watu 14 wanaotuhumiwa kwenye kashfa hiyo.
Hata hivyo Blatter alisema anatumia mamlaka aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani.

Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ili kukemea rushwa.

Mwandishi wa BBC,Nick Bryant mjini New York anasema kuwa bado maafisa hao wa marekani wana matumaini ya kupata ushirikiano kutoka kwenye takwimu za Fifa kwa sasa ili kubaini namna ambavyo mzunguko wa pesa chafu unavyomuhusisha Blatter.

Katika taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa maafisa wa Marekani wiki iliyopita kuhusu rushwa katika shirikisho hilo la soka ulimwenguni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter moja kwa moja .

Ingawa alisema kuwa huu ni mwanzo tu wa uchunguzi na si mwisho.
Mwandishi wetu anasema huu ni msingi wa maafisa wa marekani katika kuikomboa dunia katika majanga makubwa kama haya.

Mwanzoni FBI,mamlaka ya ndani ya huduma za Mapato nchini Marekani na mwanasheria wa New York , ambaye alishiriki katika uchunguzi huo walisema kuwa hawana maoni juu ya kujiuzulu kwa Blatter.

WAKALI WA TENIS KUKUTANA PARIS

 RAFAEL NADAL
Rafael Nadal bingwa mara tisa wa michuano hiyo anavaana na Djokovic mchezaji nambari moja kwa ubora. Nadal Mhispania amewahi kumshinda Mserbia Djokovic mara sita katika michuano hiyo siku za nyuma.
Huu unaelezwa kuwa mpambano mkali zaidi katika michuano ya French Open inayoendelea katika viwanja vya tenis mjini Paris ukiwemo uwanja wa Roland Garros.
Rafael Nadal
Mchezaji nambari mbili kwa ubora katika mchezo huo duniani kwa wanaume na bingwa wa mwaka 2009 Roger Federer ameng'olewa katika michunao hiyo hatua ya robo fainali baada ya kucharazwa na Stan Wawrinka kwa seti 6-4 6-3 7-6 (7-4).
Wawrinka, mwenye umri wa miaka 30, amewahi kupoteza michezo yote minne walipokutana na Federer katika michuano hiyo mikubwa.
Lakini Wawrink ambaye ni wa nane kwa ubora katika tenis amemwangusha Federer mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa mchezaji mwenza katika michuano ya Kombe la Davis.
Andy Murray
Kwa matokeo hayo Wawrinka atapambana hatua ya nusu fainali na Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga ambaye anapewa nafasi kubwa kufuatia ushindi wake dhidi ya Mjapan Kei Nishikori.
Tsonga alipata kibarua kigumu kumng'oa mpinzani wake Nishikori alipopata matokeo ya kufunga seti tatu dhidi ya mbili yaani 6-1 6-4 4-6 3-6 6-3.
Kwa upande mwingine Andy Murray leo atajaribu kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya French Open kwa mara ya tatu katika siku ambayo Novak Djokovic na Rafael Nadal wanapambana mjini Paris.
Murray wa tatu kwa ubora duniani anacheza dhidi ya Mhispania David Ferrer anayeshika nafasi ya saba kwa ubora.
Murray amesema hilo litakuwa pambano kali na mtihani mkubwa kwake.

MUZIKI WA J - LO WAZUA HISIA KALI MOROCO ....

 
J LO
 
Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa kiislamu nchini Morocco za kumtaka waziri wa mawasiliano nchini humo kujiuzulu kufuatia Tamasha la muziki lililomuhusisha msanii Jenifer Lopez mjini Rabat ambalo wamelitaja kama kuukosea adabu uma kulingana na vyombo vya habari vya taifa hilo.
J-lo kama anavyojulikana alipanda jukwaani ili kushiriki katika tamasha la muziki la Mawazine huku vyombo vya habari vya serikali vikitaja utendaji wake kama wa hali ya juu.

Lakini malalamishi yalianza baada ya J-lo kuonyeshwa katika runinga huku wito wa kujiuzulu kwa waziri huyo ukitolewa.
Hatahivyo waziri huyo amekataa kujiuzulu.

MLIPUKO WA BOMU NIGERIA WAUA WATU 20 ...!

 
Takriban watu 20 wamefariki kutokana na mlipuko wa bomu katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.
Mji huo ulikuwa umeshambuliwa saa za alfajiri siku ya jumanne na washukiwa wa kundi la Boko haram .

Saa chache baadaye ,mlipuaji wa kujitolea muhanga alijilipua katika soko la kuuza ngombe la Gamboru ndani ya mji huo kulingana na walioshuhudia.
Wakati wa kuapishwa kwake rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema kuwa anayahamisha makao makuu ya kijeshi katika vita dhidi ya wapiganaji hao kutoka mji mkuu wa Abuja hadi Maiduguri.

KUKOSEKANA USALAMA BURUNDI SHUGHULI ZAKWAMA ....

Hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi imeendelea kuwa tete. Uchaguzi wa Wabunge na Madiwani umekua unatazamiwa kufanyika rasmi Ijumaa Juni 5, lakini sasa haijulikani iwapo utafanyika au la.

    

Jumapili Mei 31, viongozi wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki walikutana na kuchukua uamzi wa kuitaka serikali ya Burundi na Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) kuahirisha kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu uchaguzi huo.

Tume Huru ya Uchaguzi, kwa upande wake, imeendelea kuhakikisha kuwa inaendesha kazi yake kama kawaida licha ya kujiuzulu kwa naibu mwenyekiti wa Tume hiyo, Spes-Caritas Nirondoye, pamoja na mkurugenzi wa masuala ya utawala na fedha, Illuminata Ndabahagamiye. Lakini kujiuzulu kwa watu hao ni tatizo kubwa kwa utendaji kazi wa Tume hiyo ya Uchaguzi.

Hakuna matatizo yoyote kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi. Rais Nkurunziza anatazamiwa kusaini sheria baada ya kukutana na kushauriana na Tume huru ya Uchaguzi (Ceni). Iwapo kuahirishwa kutathibitishwa, kuahirishwa kwa uchaguzi kutatangazwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Hata hivyo tume huru ya Uchaguzi bado inakabiliwa na matatizo ya utendaji kazi, baada ya kujiuzulu kwa wajumbe wake wawili kwa jumla ya wajumbe watano wanaounda Tume hiyo.

Hata hivyo, Tume huru ya Uchaguzi inapaswa kuchukua maamuzi ya kuandaa uchaguzi kwa makubaliano ya wajumbe wote au kwa idadi kubwa ya wajumbe 4 kwa jumla ya watano wanaounda Ceni.

Kutokana na hali hiyo italazimika kuwateua watu wengine wawili watakaochukua nafasi ya wajumbe hao wawili waliojiuzulu. Na kwa mujibu wa Katiba, inahitaji sheria ya rais baada ya watu hao kupasishwa kwa asilimia 75 ya Wabunge na Maseneta.

Wabunge na maseneta wameanza kukutana katika vikao mbalimbali tena kuanzia Jumatatu, Juni 1, zikisalia siku 3 za uchaguzi wa wabunge na Madiwani kufanyika kulingana na kalenda ya uchaguzi ya zamani. Hali hii imewashangaza wengi wakati Baraza la Bunge na Seneti vilimaliza muhula wao tangu Aprili 30.

Kinachosalia ni kujua iwapo serikali itafanikiwa kukusanya asilimia 75 za kura kwa kuweza kuwapitisha wagombea hao kwenye nafasi za wajumbe wa Ceni waliojiuzulu, hasa kwa upande wa Baraza la Bunge.

BREAKING NEWS : SEPP BLATA AMEJIUZULU U RAIS WA FIFA ..

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter Kujiuzulu
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa atajiuzulu kama rais wa shirikisho hilo kufuatia kashfa ya ufisadi.
Akitangaza kujiuzulu,kwake Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameitisha kikao cha dharura mara moja ili kumchagua rais mpya.
Blatter alichaguliwa tena wiki iliopita licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi .
Lakini alisema kuwa mamlaka yake hayaungwi mkono na kila mtu.Shirikisho la FIFA lilikumbwa na mgogoro wa kukamatwa kwa maafisa wake kutokana na mashtaka ya ufisadi ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa na marekani .
Uchunguzi mwengine unaofanywa na serikali ya Switzerland kuhusu vile michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 na 2022 ilitolewa pia unaendelea.''Nimehusika sana na FIFA na maslahi yake.Kilicho muhimu kwangu ni taasisi ya FIFA na Soka duniani''