Thursday, 5 March 2015
KISA CHA UJAMBAZI WA AKILI NYINGI KONA BAA .. HILI SIO TUKIO LA KIJAMBAZI .. THIS WAS A MISSION With too much brain ( akili nyingi kwa kiswahili )
TUKIO hili limetokea siku kidogo hapa dar na hizi baa zipo sinza dar es salaam ...
Niliahidi moyoni jana kua leo ningejitahidi kuiacha stori hii itawale leo siku nzima na ninadhani itakua hivyo ..
Oi .. stori ni ndefu nitaifupisha sana ili kuokoa muda wako na pia nitajitahidi ilete maana ile ile .
SOMO ...
Pale kona baa na kangaroo sinza waliopo kazini pale kuuza kwichi kwichi huwaita wanaume wanaonunua WACHATI , ... na kile kitendo cha kwichi kwichi huitwa KUCHETUANA ..
Kuna dem anaitwa ANNA huyu dem ni mruwanda ila anauza kwich kwich pale kona baa , mimi sikua namjua wala sikutaarifiwa kuwapo kwake wala stori yake ila niliitwa kumsikiliza msela mmoja anaitwa Macho ambae pia utamsoma siku si nyingi ..,, tukiwa tumekaa maskani moja pale kona baa namsikiliza masela akaja dem mzuri tu japo bonge kidogo ila anavutia ,..
Akatusalimia tukazoeana kwa muda mfupi , yeye yule dem anachetuana na mshkaji wa Macho anaitwa Frank .. baada ya story story pale na Macho dem akajikuta anafunguka :
... Anna : Niwape kisa changu ambae sijawai kumwambia mtu yeyote ( hajui kiswahili vyema )
... Mimi Funguka mama ..
Anna : kicheko kidogo kisha akaanza ...
Kuna siku nilikua humu ndani ( baa kangaroo ) akaja mkaka mmoja akanikuta kaunta , akanisalimia vizuri kiheshima akavuta kiti akakaa anaonekana mstaarabu tu sana , kaniuliza unakunywa nini nikaagiza bia ya kwanza , ya pili, ya tatu akaja jamaa mwingine akatusalimia nae akakaa karibu yetu akaagiza bia ila akatoa laki akaweka mezani akaniambia tuondoke mi nikafikiri utani nikacheka yule wangu akaweka laki mbili nikashangaa. . . Mara na yule akapanda dau akaweka kama cjui laki ngapi ila nyingi , yule wangu akaongeza yule jamaa akachukia akatukana akaondoka zile pesa zipo pale pale ... yule wa mwanzo akaniambia chukua hizo pesa weka kwenye pochi yako ... nikazichukua nikaziweka zote kwenye pochi .. akaniambia malizia bia yako tuondoke hapa sio pazuri poa ,, mi fasta nikamalizia bia tukaenda kwenye gari na yule kaka ila kulikua na wa kaka wengine watatu pamoja na yuulee .. mi nikakaa upande wa dirisha .. tukaenda mpaka sheli wakanipa hela niweke mafuta mi nikashusha kioo nikamwambia mdada wa sheli weka full tank .. alipomaliza nataka kumpa hela akawa kashikilia hela zingine nyingi mkononi anasubiri nimpe pesa ya mafuta sasa .. wale watu mmoja akashuka anasema kaeni kama mlivyo nisiskie sauti naua mmoja mkononi anabastola saa hiyo hiyo wanaingia ndani pale kwa dukani ya supermarket wanatoka na ma box wanaweka huko nyuma .. mimi naogopa lakini sio sana ( dem kaona baba yao na mlinzi wanachinjwa huko kwao na amekaa na maiti saana) ... basi wakaenda sheli ya pili ila pale hawakukaa sana tukaondoka .. wakawa wanaisimulia maisha alakini mi siwaelewi .. kushtuka tupo poriini saana silewi tunakokwenda ila siwezi kuuliza ni wapi ... wakaeendaa wakasimama poriini hatasijui wapi ... wakanishusha .. zile hela walizonipa pale baa niliweka kwenye pochi ... pochi wameninyang'anya kulikua na hela yangu sio zile zao nyingi yangu ilikua elfu 12 na cm yangu .. wakatoa hela zao wakaweka cm yangu wakanipa pochi ina elfu 12 wakaniambia weka kichwa chini na usinyanyuke tunakuwekea bomu ukinyanyua kichwa tu umekufa.. Anna anakwambia akasujudu pale kama masaa matatu sasa kachoka anaumia kuinua kichwa taratibu asikie puuuuu kalipuka ... mbele akaona majani yatikisika akajua nyoka akaruka kwa mshtuko mara mgongoni anaangusha parachichi aliloambiwa ni bomu ...
Anaangalia yupo wapi hajui gizaa la hatari sasa anatafuta bara bara hajui ipo wapi na yeye mwenyewe kuachwa wapi ... akafanikiwa kuiona bara bara asubuhi .. akamuuliza msamaria hapa wapi akaambiwa mdaulah ... Anna akauliza ndio wapi ?? Akaambiwa jirani na morogoro akauliza nauli mpaka dar sh. Ngapi akaambiwa elfu 8 .. akamwambia kaka naomba nipeleke kwenye napata gari ya kurudi dar .
DYU .. ni nomaa..
Fikiria vijana wanavyotumia akili katili kufanya yao ... tunawataka watumie akili hizi tuendeleze taifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.jpg)
No comments:
Post a Comment