Leo ni siku ya wanyama na mazao ya
porini duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka
umakini zaidi katika kushughulikia vitendo vya uhalifu dhidi ya
maliasili hiyo.
Amesema kushamiri huko kunapigiwa chepuo na rushwa na uongozi dhaifu akiongeza kuwa kuna ushahidi thabiti wa kuhusika kwa mitandao ya kihalifu iliyopangwa na vikundi vilivyojihami.
Ban amesema biashara hiyo haramu siyo tu inakwamisha utawala wa sheria bali pia unatishia usalama wa taifa na ni kikwazo kikubwa kwa juhudi za wanavijiji na jamii za watu wa asili za matumizi endelevu za maliasili.
Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu ametaka umakini wa kushughulikia uhalifu huo akitaka ushiriki wa jamii zote zinazohusika na matumizi ya maliasili hizo kwa ajili ya dawa, chakula, ujenzi, samani, urembo na nguo.
Amesema endapo usimamizi wa sheria utakwenda sambamba na ushirikishi wa jamii nzima kutawezesha kumaliza tatizo la matumizi haramu ya bidhaa za porini.
MAKAO MAKUU YA NCHI YETU PANAPOSHUGHULIKA NA HAYA NI HAPA : >
Makao MAKUU ya wizara ya NYALANDU mali asili na UTALII ..
picha zote MBILI kwa hisani ya Tutoke Vipi
No comments:
Post a Comment