Wapiganaji wa kiislamu wameripotiwa
kuviteka visima viwili vya mafuta katikati mwa Libya huku makundi hasimu
yakiendelea kupigania udhibiti wa taifa hilo.
Serikali ya Libya inayotambulika kimataifa mjini Tobruk inakabiliana na mahasimu wake wa Libya Dawn ambao wanadhibiti mji mkuu wa Tripoli.
Pande hizo mbili pia zilishambuliana siku ya jumanne.
''Watu wenye itikadi kali walichukuwa udhibiti wa maeneo ya al Bahi na al Mabruk na sasa wanaelekea kudhibiti kisima cha mafuta cha Al Dahra kufuatia kusalimu amri kwa vikosi vilivyokuwa vikilinda maeneo hayo'',alisema kanali al_Hassi, msemaji wa usalama wa sekta ya mafuta.
No comments:
Post a Comment