Mamia ya raia wa Zimbambwe
wameandamana nje ya ubalozi wa Afrika Kusini mjini Harare wakitaka
kusitishwa kwa mashambulizi yanayoendeshwa dhidi ya wahamiaji nchini
Afrika kusini.
Maelfu ya Wazimbabwe huishi na kufanya kazi nchini Afrika Kusini ambapo takriban watu watano wameuawa kwenye mashambulizi yanayowalenga wageni.
Ghasia hizo zilianza baada ya mfalme wa zulu Goodwill Zwelethini kusema kuwa wageni ni lazima waondoke Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment