Monday, 11 May 2015

NDANDA WAMALIZA NYODO ZA SIMBA ...>>

NDANDA FC ya mjini Mtwara imefanikiwa kuepuka kushuka daraja baada ya kuifunga Yanga bao 1-0 juzi Jumamosi, lakini gumzo kubwa kwa timu hiyo ni kuvunja rekodi ya Simba.
Ushindi huo wa Ndanda mbele ya Yanga umeifanya kuwa timu ya pili kuweza kuzifunga Yanga na Azam msimu huu rekodi ambayo Simba walikuwa wakijivunia nayo na kutoa maneno ya kejeli kila kona.
Ndanda iliifunga Azam bao 1-0 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa Mtwara, Oktoba mwaka jana na kisha kuifunga Yanga juzi Jumamosi.

 

Simba nayo iliifunga Yanga bao 1-0 mapema Machi kabla ya kuifunga Azam 2-1 mapema mwezi huu na kujivunia rekodi ya kupata matokeo mbele ya timu hizo mbili zilizomaliza katika nafasi mbili za juu za Ligi Kuu Bara, rekodi ambayo pia Ndanda imeiweka.
Timu nyingine ambazo zilikaribia kuweka rekodi hiyo ni Mtibwa Sugar ambayo iliifunga Yanga mara moja, Kagera Sugar iliyoifunga pia Yanga mara moja na JKT Ruvu iliyoifunga Azam mara moja. Wengine walitoa sare au kufungwa.

No comments:

Post a Comment