Polisi mjini Texas wanasema kuwa
wamewapiga risasi na kuwaua watu wawili waliokuwa na silaha,
waliowashambulia walinda usalama kwa risasi, walipofika katika eneo la
hafla moja yenye utata ya uchoraji wa vibonzo vya kuwakejeli waislamu na
mtume Mohammed.
Hafla za Sherehe hiyo iliyoandaliwa na kundi moja la kisiasa la kihafidhina, ambalo limekuwa likikejeli Uislamu, lilikuwa litoe zawadi nono ya dola milioni kumi kwa mchoraji kibonzo mahiri zaidi, atakayeibuka mshindi kwa kumchora mtume Mohamed.
Kikosi cha kutegua mabomu pamoja na ndege za helikopta za polisi zimefika mahali hapo kwa sasa.
No comments:
Post a Comment