Shirika la India linalohusika na
ubora wa vyakula limepiga marufuku utengenezaji wa chakula aina ya tambi
ziitwazo ''Maggi Noodles'' baada ya kugunduliwa kuwa na kiwango kikubwa
cha madini hatari aina ya lead.
Kulikuwa na aina tisa ya ''Maggi Noodles'', bidhaa iliyotokea kushabikiwa na walaji wengi hivyo kununuliwa kwa wingi.Bidhaa hiyo inashikilia asilimia 80% ya soko la tambi nchini humo.
Wakati huohuo Singapore imesitisha mauzo ya tambi hizokutoka india nchini mwao.
Kufuatia tukio hilo soko la tambi za Nestle limeporomoka huko India .
No comments:
Post a Comment