Vitendo vya kikatili na unyanyasaji wa Wanawake na watoto vinaendelea
kushika kasi licha ya Serikali na mashirika mbalimbali ya haki za
Binadamu kupiga vita vitendo hivyo kwa nguvu .
Hali hiyo imejitokeza katika kijiji cha Kasaka, Kata ya Nyaruyoba Wilaya
ya Kibondo mkoani Kigoma baada ya Baba mzazi aliyefahamika kwa jina la
Sindotuma Nyamubi, kumchoma moto na kumuunguza vibaya sehemu za mdomoni
wake, mtoto wake wa miaka saba akimtuhumu kudokoa maharage yaliyotakiwa
kutumika kama mboga kwa ajili ya kulia chakula.
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwa Felix Cosmas amesema kuwa mtoto huyo
alibainika kuwa amefanyiwa kitendo hicho baada ya majirani kutomuoana
akicheza na wenzake kwa muda wa siku tatu kama ilivyokuwa imezoeleka,
ndipo walipogundua alikuwa amefichwa ndani ya nyumba na kugundua tatizo
hilo na kutoa taarifa hatua iliyofanikisha mzazi huyo kukamatwa na
kufikishwa Polisi.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Kibondo,Bi Sofia Gwamagobe amesema
kuwa ni vizuri wazazi na walezi kutambua na kujali hali za watoto na
sambamba na jamii pia kuendelea kufichua na kutoa taarifa katika vyombo
husika ili kuweza kuokoa maisha ya watu wanaofanyiwa mambo kama hayo
kama wamejeruhika kuwapatia matibabu kabla hawajapata madhara makubwa
Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Kibondo, amekiri kuwepo kwa tukio hilo,
na kumtaja aliyejeruhiwa vibaya kuwa ni Shukuru Sindotuma na amesema
baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa kituoni hapo, amekubali kuwa
alimchoma moto mtoto wake kwa kosa la kula maharage bila ruhusa yake
Mtoto huyo Shukuru Sindotuma alikuwa anaishi na baba yake ,mdogo wake mmoja huku Wazazi wao wakiwa wametengana

No comments:
Post a Comment