Tuhuma: Taarifa zilizofikia Raia Mwema kutoka ndani ya kikao hicho, zimemtaja mjumbe aliyenusurika kuchapwa makonde na mbunge huyo kuwa ni Simon Mahenge ambaye pia ni Katibu wa CCM Kata ya Bagara na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Habari hizo zilieleza kuwa Chambiri alifikia hatua ya kutaka kumchapa makonde mjumbe huyo baada ya “kukasirishwa” na hoja zake kuwa mbunge huyo ni chanzo cha mpasuko mkubwa unaokikabili chama hicho, kufanya vikao usiku na kuwasadia wapinzani katika uchaguzi huo. “Wakati Mwenyekiti (Ally Msuya) alipofungua kikao na kuruhusu wajumbe kuanza kujadili ajenda, alisimama Mzee Mahenge ambaye alianza kwa kumtuhumu Chambiri kuwa ni chanzo cha mpasuko ulioikumba chama hicho kwa tabia yake ya kuwagawa wanachama katika ngazi ya mashina, matawi, kata na hata wilaya,”alieleza mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao hicho. Akimkariri Mahenge, mjumbe huyo aliongeza:”Tatizo la CCM Babati ni kuwa na mbunge ambaye anagawa wanachama, kwa kufanya vikao usiku na wanawake, badala ya kuwasiliana na viongozi wa kata husika, na pia amehusika kutuhujumu katika baadhi ya mitaa kwa kuwasadia kifedha wagombea wa vyama vya upinzani katika uchaguzi wa serikali za mitaa”. Mjumbe huyo aliongeza kuwa kufuatia tuhuma hizo, Chambiri aliinuka alipokuwa amekaa na kwenda kumvamia mzee Mahenge akiwa amekunja ngumi tayari kwa mapambano na kumkunja shati. Hatua hiyo inaelezwa kuwashangaza wajumbe ambapo baadhi ya viongozi walioko meza kuu wakioongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Mohamed Farah ambao waliingilia kati na kuamua. “Hali ilikuwa inatisha ndani ya kikao na wajumbe walipigwa na mshangao mkubwa kwamba Mbunge badala ya kusubiri muda wake ajibu hoja alikimbilia kutaka kumpiga mjumbe mwenzake kinyume na utaratibu wa vikao katika chama chetu,”aliongeza mjumbe huyo.
Akizungumza na Raia Mwema, Mzee Mahenge alithibitisha kuwa ni kweli Mbunge Chambiri alitaka kumshambulia ndani ya kikao hicho baada ya kutoa hoja za kumtuhumu kuwa ni tatizo kubwa na anakigawa chama chao. “Madai yangu ni ya kweli na nina vielelezo vyote, nisingweza kumtuhumu mbunge wa chama changu bila ya sababu.
Kero za wananchi zimekuwa nyingi, yeye pamoja na baadhi ya madiwani wameshindwa kuzitatua na hali hiyo inafanya chama chetu kionekane mzigo mbele ya wananchi”alisema. “Kwa mfano kuna migogoro ya ardhi katika kata yangu ya Bagara katika maeneo ya Negamsi, Miomboni, Bagara Ziwani na Komoto tangu mwaka 2010 lakini Mbunge haonekani jimboni wala hajawahi kushughulikia migogoro hiyo ambayo inahatarisha usalama,”alisema Mahenge.
Aliongeza kuwa katika baadhi ya maeneo hayo, ardhi ya wananchi ilimegwa kwa ajili ya huduma za kijamii kama ujenzi wa kituo cha polisi na serikali imelipa fidia ya shilingi milioni 76, na hadi sasa fedha hizo hazijawafikia walengwa. “Tunaelekea katika uchaguzi mkuu mwaka huu, je tutaenda kuwaambia nini wananchi wa jimbo la Babati Mjini? Mbunge wetu ambaye hajatekeleza ahadi zake nyingi badala ya kuja kwa viongozi wa kata na matawi kufanya vikao anakutana na baadhi ya wanachama usiku kufanya vikao, kinyume cha kanuni na sheria za nchi,”alisema. Mahenge alisema kuwa atashangazwa sana na viongozi wa CCM iwapo hawatachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mbunge huyo ambaye anadaiwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwatishia usalama wanachama ambao hawamwungi mkono katika harakati zake za kisiasa. Viongozi wazungumza: Akizungumzia sakata hilo, Katibu wa CCM Wilaya ya Babati, Daniel ole Porokwa alithibitishia Raia Mwema kuwa tukio hilo lilitokea na chama chake kitafanyia kazi suala hilo. Katibu huyo wa CCM alieleza kuwa pamoja na Chambiri, hatua hizo zitachukuliwa pia dhidi ya wanachama ambao wamekiuka kanuni na maadili ya chama hicho akiwemo Katibu Mwenezi wa wilaya Reginald Sanka. “Sitaki kuingia kwa undani suala hilo mchakato wake uko katika hatua za awali, tutayafanyia kazi mambo yote hayo ili kukijenga chama chetu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu,”alisema ole Porokwa. Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Babati, Ally Msuya, pamoja na kuthibitisha suala hilo, aliongeza kuwa alitumia mamlaka yake kama Mwenyekiti kumnusuru mjumbe aliyetaka kupigwa. “Ni jambo la kufedhehesha sana, huu si utamaduni wa CCM wa wajumbe kupigana au kutumia lugha chafu ndani ya vikao, nilitumia mamlaka yangu kama Mwenyekiti kumkanya Mbunge kuwa amefanya makosa makubwa sana,”alisema. Mwenyekiti huyo wa CCM alikiri kuwa kuna mpasuko ndani ya chama hicho na chanzo chake ni tabia ya Mbunge Chambiri kuwagawa wanachama kutokana na baadhi kutotaka kumwunga mkono katika harakati za kutetea kiti chake. “Tumemwonya kuhusu tabia yake ya kufanya vikao usiku katika maeneo mengi, baadhi ya wanaoshiriki vikao hivyo ni wanawake ambao ni wake za watu. Sasa jiulize, unakaa vikao na wake za watu hadi usiku wa manane kwanini?aina hii ya siasa haikubaliki ndani ya CCM hasa Babati,”alisema.
Msuya aliongeza:”Tufahamu kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, na si vibaya wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kupitia chama chetu kuwafikia wanachama, lakini si kwa mbinu hizi za kufanya vikao vya usiku vinavyotishia ndoa za wanachama wetu”.
Mwenyekiti huyo anatoa wito kwa wanachama wa CCM katika jimbo lake kuwa makini sana na mienendo ya wagombea wa nafasi za uongozi ambao wamekuwa wanagawa fedha kwa wanachama, ili wapigiwe kura muda wa uchaguzi utakapowadia. “Tabia hii ya kupokea fedha au kudai fedha kutoka kwa watangaza nia ni kuendekeza rushwa na hii ni kansa itakayoangamiza chama chetu. Wito wangu ni kwamba wanachama wazingatia vigezo vya kiongozi bora badala ya vishawishi wa fedha,”alisema. Chambiri ajibu tuhuma:Akijibu madai yanayotolewa dhidi yake, Chambiri alikanusha kuwa alifikia hatua ya kutaka kumtia makonde mjumbe alikuwa anamtuhumu ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya Januari 26 mwaka huu. “Kama jambo hilo lina ukweli basi litakuwa miongoni mwa maazimio ya kikao hicho. Hata hivyo hakuna azimio lolote lilolotolewa dhidi yangu baada ya mkutano huo na mimi sitambui tuhuma na madai hayo,”alisema. Kuhusu kufanya vikao usiku, Chambiri alifafanua kuwa wanachama wengi wa jimbo lake ni wakulima na si rahisi kupatikana mchana kwa kuwa wengi wanakuwa katika shughuli za kilimo. “Kwanza utambue kuwa mimi ni mbunge halali wa jimbo la Babati Mjini, hakuna sheria inayonizuia kukutana na wananchi wangu muda wowote. Lakini pia, wanachama na wananchi wengi wa jimbo langu ni wakulima ambao mchana wako katika shughuli za uzalishaji hivyo nalazimika kukutana nao usiku na sivunji sheria ya nchi,”alisema Chambiri. Chambiri aliibuka katika siasa za jimbo la Babati mwaka 2010 kama ‘mtu wa kuja’ baada ya kumwangusha Kwaang’w aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa muda wa miaka 15.
Chambiri aliwahi pia kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara. Mbunge huyo anachukuliwa kama mtu wa kuja kutokana na msingi kuwa si mwenyeji wa jimbo hilo na aliibukia Babati baada ya kampuni yake ya ukandarasi kushinda zabuni ya kutengeneza barabara inayounganisha wilaya za Simanjiro na Kiteto na makao makuu ya mkoa wa Manyara. Wanachama watadharisha: Baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM katika jimbo hilo wanatadharisha kuwa chama hicho kitakuwa katika hatari ya kupoteza jimbo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu iwapo wanachama hawatakuwa makini wakati wa kura za maoni.
Mwenyekiti wa CCM tawi la Negamsi, John Anney Bura, alitahadharisha chama hicho kinaweza kupoteza jimbo hilo iwapo wanachama hawatakuwa makini wakati wa uchaguzi kura za maoni. “Kwanza kuna suala la matumizi makubwa ya fedha kutoka kwa baadhi ya watangaza nia jambo ambalo linahatarisha mshikamano ndani ya CCM kwa sababu si wanachama wote wanafikiwa na fedha za rushwa”alisema. Naye Katibu wa CCM Kata ya Babati Mjini, Omar Hussein alisema wanachama wa CCM wanapaswa kubadilika na kuachana na tabia ya kuwachagua viongozi kwa vigezo vya fedha.
Mgombea wa CCM atakayeshinda kura za maoni pia atakuwa na mtihani mgumu wa kupambana na nguvu ya muungano wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao wanatarajia kumpitisha Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Paulina Gekul. - See more at: http://www.raiamwema.co.tz/mbunge-atembeza-ngumi-kikaon
MBUNGE
wa Jimbo la Babati Mjini (CCM), Kiseryi Chambiri, ameingia matatani
baada ya kutuhumiwa kutaka kumchapa makonde mjumbe mmoja wa Halmashauri
Kuu ya wilaya hiyo (NEC) ndani ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na na viongozi wa wilaya hiyo,
limetokea Januari 26 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa jengo la CCM
mjini Babati, wakati wajumbe wa Halmashauri Kuu hiyo wakijadili ajenda
ya tathamini ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14
mwaka jana.
Aidha tukio hilo pia linahusishwa na harakati za uchaguzi mkuu
utakaofanyika baadaye mwaka huu, ambapo taarifa zinadai kuwa Chambiri
anakabiliwa na upinzani mkali ndani ya chama chake na uwezekano wa
kurudi bungeni unaelezwa kuwa “finyu” sana.
Inadaiwa kuwa, Chambiri, kwa muda mrefu amepoteza ushawishi kwa
wananchi, wanachama na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Babati kutokana na
kile kinachoelezwa kuwagawa wanachama wa CCM katika makundi tangu
alipoingia bungeni mwaka 2010 baada ya kumwangusha aliyekuwa Mbunge wa
jimbo hilo, Omar Kwaang’w.
Taarifa zinadai kuwa tayari wachama 13 wa CCM wameonyesha nia ya
kukabiliana na Chambiri katika hatua za mchujo wa ndani ya chama na hali
hiyo imesababisha mbunge huyo kukosa “usingizi” na kuanza kuhaha
kuokoa kiti chake.
Tuhuma:
Taarifa zilizofikia Raia Mwema kutoka ndani ya kikao hicho, zimemtaja
mjumbe aliyenusurika kuchapwa makonde na mbunge huyo kuwa ni Simon
Mahenge ambaye pia ni Katibu wa CCM Kata ya Bagara na Mjumbe wa Mkutano
Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Habari hizo zilieleza kuwa Chambiri alifikia hatua ya kutaka kumchapa
makonde mjumbe huyo baada ya “kukasirishwa” na hoja zake kuwa mbunge
huyo ni chanzo cha mpasuko mkubwa unaokikabili chama hicho, kufanya
vikao usiku na kuwasadia wapinzani katika uchaguzi huo.
“Wakati Mwenyekiti (Ally Msuya) alipofungua kikao na kuruhusu wajumbe
kuanza kujadili ajenda, alisimama Mzee Mahenge ambaye alianza kwa
kumtuhumu Chambiri kuwa ni chanzo cha mpasuko ulioikumba chama hicho
kwa tabia yake ya kuwagawa wanachama katika ngazi ya mashina, matawi,
kata na hata wilaya,”alieleza mmoja wa wajumbe waliohudhuria kikao
hicho.
Akimkariri Mahenge, mjumbe huyo aliongeza:”Tatizo la CCM Babati ni kuwa
na mbunge ambaye anagawa wanachama, kwa kufanya vikao usiku na wanawake,
badala ya kuwasiliana na viongozi wa kata husika, na pia amehusika
kutuhujumu katika baadhi ya mitaa kwa kuwasadia kifedha wagombea wa
vyama vya upinzani katika uchaguzi wa serikali za mitaa”.
Mjumbe huyo aliongeza kuwa kufuatia tuhuma hizo, Chambiri aliinuka
alipokuwa amekaa na kwenda kumvamia mzee Mahenge akiwa amekunja ngumi
tayari kwa mapambano na kumkunja shati.
Hatua hiyo inaelezwa kuwashangaza wajumbe ambapo baadhi ya viongozi
walioko meza kuu wakioongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa
Babati, Mohamed Farah ambao waliingilia kati na kuamua.
“Hali ilikuwa inatisha ndani ya kikao na wajumbe walipigwa na mshangao
mkubwa kwamba Mbunge badala ya kusubiri muda wake ajibu hoja alikimbilia
kutaka kumpiga mjumbe mwenzake kinyume na utaratibu wa vikao katika
chama chetu,”aliongeza mjumbe huyo.
Akizungumza na Raia Mwema, Mzee Mahenge alithibitisha kuwa ni kweli
Mbunge Chambiri alitaka kumshambulia ndani ya kikao hicho baada ya kutoa
hoja za kumtuhumu kuwa ni tatizo kubwa na anakigawa chama chao.
“Madai yangu ni ya kweli na nina vielelezo vyote, nisingweza kumtuhumu
mbunge wa chama changu bila ya sababu. Kero za wananchi zimekuwa nyingi,
yeye pamoja na baadhi ya madiwani wameshindwa kuzitatua na hali hiyo
inafanya chama chetu kionekane mzigo mbele ya wananchi”alisema.
“Kwa mfano kuna migogoro ya ardhi katika kata yangu ya Bagara katika
maeneo ya Negamsi, Miomboni, Bagara Ziwani na Komoto tangu mwaka 2010
lakini Mbunge haonekani jimboni wala hajawahi kushughulikia migogoro
hiyo ambayo inahatarisha usalama,”alisema Mahenge.
Aliongeza kuwa katika baadhi ya maeneo hayo, ardhi ya wananchi ilimegwa
kwa ajili ya huduma za kijamii kama ujenzi wa kituo cha polisi na
serikali imelipa fidia ya shilingi milioni 76, na hadi sasa fedha hizo
hazijawafikia walengwa.
“Tunaelekea katika uchaguzi mkuu mwaka huu, je tutaenda kuwaambia nini
wananchi wa jimbo la Babati Mjini? Mbunge wetu ambaye hajatekeleza ahadi
zake nyingi badala ya kuja kwa viongozi wa kata na matawi kufanya vikao
anakutana na baadhi ya wanachama usiku kufanya vikao, kinyume cha
kanuni na sheria za nchi,”alisema.
Mahenge alisema kuwa atashangazwa sana na viongozi wa CCM iwapo
hawatachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mbunge huyo ambaye anadaiwa
kuwa amekuwa na tabia ya kuwatishia usalama wanachama ambao hawamwungi
mkono katika harakati zake za kisiasa.
Viongozi wazungumza:
Akizungumzia sakata hilo, Katibu wa CCM Wilaya ya Babati, Daniel ole
Porokwa alithibitishia Raia Mwema kuwa tukio hilo lilitokea na chama
chake kitafanyia kazi suala hilo.
Katibu huyo wa CCM alieleza kuwa pamoja na Chambiri, hatua hizo
zitachukuliwa pia dhidi ya wanachama ambao wamekiuka kanuni na maadili
ya chama hicho akiwemo Katibu Mwenezi wa wilaya Reginald Sanka.
“Sitaki kuingia kwa undani suala hilo mchakato wake uko katika hatua za
awali, tutayafanyia kazi mambo yote hayo ili kukijenga chama chetu
kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu,”alisema ole Porokwa.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Babati, Ally Msuya, pamoja na
kuthibitisha suala hilo, aliongeza kuwa alitumia mamlaka yake kama
Mwenyekiti kumnusuru mjumbe aliyetaka kupigwa.
“Ni jambo la kufedhehesha sana, huu si utamaduni wa CCM wa wajumbe
kupigana au kutumia lugha chafu ndani ya vikao, nilitumia mamlaka yangu
kama Mwenyekiti kumkanya Mbunge kuwa amefanya makosa makubwa
sana,”alisema.
Mwenyekiti huyo wa CCM alikiri kuwa kuna mpasuko ndani ya chama hicho na
chanzo chake ni tabia ya Mbunge Chambiri kuwagawa wanachama kutokana na
baadhi kutotaka kumwunga mkono katika harakati za kutetea kiti chake.
“Tumemwonya kuhusu tabia yake ya kufanya vikao usiku katika maeneo
mengi, baadhi ya wanaoshiriki vikao hivyo ni wanawake ambao ni wake za
watu. Sasa jiulize, unakaa vikao na wake za watu hadi usiku wa manane
kwanini?aina hii ya siasa haikubaliki ndani ya CCM hasa Babati,”alisema.
Msuya aliongeza:”Tufahamu kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi, na si vibaya
wenye nia ya kugombea nafasi za uongozi kupitia chama chetu kuwafikia
wanachama, lakini si kwa mbinu hizi za kufanya vikao vya usiku
vinavyotishia ndoa za wanachama wetu”.
Mwenyekiti huyo anatoa wito kwa wanachama wa CCM katika jimbo lake kuwa
makini sana na mienendo ya wagombea wa nafasi za uongozi ambao wamekuwa
wanagawa fedha kwa wanachama, ili wapigiwe kura muda wa uchaguzi
utakapowadia.
“Tabia hii ya kupokea fedha au kudai fedha kutoka kwa watangaza nia ni
kuendekeza rushwa na hii ni kansa itakayoangamiza chama chetu. Wito
wangu ni kwamba wanachama wazingatia vigezo vya kiongozi bora badala ya
vishawishi wa fedha,”alisema.
Chambiri ajibu tuhuma:Akijibu madai yanayotolewa dhidi yake, Chambiri
alikanusha kuwa alifikia hatua ya kutaka kumtia makonde mjumbe alikuwa
anamtuhumu ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya Januari 26 mwaka
huu.
“Kama jambo hilo lina ukweli basi litakuwa miongoni mwa maazimio ya
kikao hicho. Hata hivyo hakuna azimio lolote lilolotolewa dhidi yangu
baada ya mkutano huo na mimi sitambui tuhuma na madai hayo,”alisema.
Kuhusu kufanya vikao usiku, Chambiri alifafanua kuwa wanachama wengi wa
jimbo lake ni wakulima na si rahisi kupatikana mchana kwa kuwa wengi
wanakuwa katika shughuli za kilimo.
“Kwanza utambue kuwa mimi ni mbunge halali wa jimbo la Babati Mjini,
hakuna sheria inayonizuia kukutana na wananchi wangu muda wowote. Lakini
pia, wanachama na wananchi wengi wa jimbo langu ni wakulima ambao
mchana wako katika shughuli za uzalishaji hivyo nalazimika kukutana nao
usiku na sivunji sheria ya nchi,”alisema Chambiri.
Chambiri aliibuka katika siasa za jimbo la Babati mwaka 2010 kama ‘mtu
wa kuja’ baada ya kumwangusha Kwaang’w aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
kwa muda wa miaka 15.
Chambiri aliwahi pia kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara.
Mbunge huyo anachukuliwa kama mtu wa kuja kutokana na msingi kuwa si
mwenyeji wa jimbo hilo na aliibukia Babati baada ya kampuni yake ya
ukandarasi kushinda zabuni ya kutengeneza barabara inayounganisha
wilaya za Simanjiro na Kiteto na makao makuu ya mkoa wa Manyara.
Wanachama watadharisha:
Baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM katika jimbo hilo wanatadharisha
kuwa chama hicho kitakuwa katika hatari ya kupoteza jimbo katika
uchaguzi mkuu wa mwaka huu iwapo wanachama hawatakuwa makini wakati wa
kura za maoni.
Mwenyekiti wa CCM tawi la Negamsi, John Anney Bura, alitahadharisha
chama hicho kinaweza kupoteza jimbo hilo iwapo wanachama hawatakuwa
makini wakati wa uchaguzi kura za maoni.
“Kwanza kuna suala la matumizi makubwa ya fedha kutoka kwa baadhi ya
watangaza nia jambo ambalo linahatarisha mshikamano ndani ya CCM kwa
sababu si wanachama wote wanafikiwa na fedha za rushwa”alisema.
Naye Katibu wa CCM Kata ya Babati Mjini, Omar Hussein alisema wanachama
wa CCM wanapaswa kubadilika na kuachana na tabia ya kuwachagua viongozi
kwa vigezo vya fedha.
Mgombea wa CCM atakayeshinda kura za maoni pia atakuwa na mtihani mgumu
wa kupambana na nguvu ya muungano wa vyama vya upinzani vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao wanatarajia kumpitisha Mbunge
wa Viti Maalumu (Chadema) Paulina Gekul.
- See more at:
http://www.raiamwema.co.tz/mbunge-atembeza-ngumi-kikaoni#sthash.Zhr82FpU.dpuf

No comments:
Post a Comment