Serikali ya Tanzania imesitisha
matumizi ya tiketi za elektroniki ( kununua kwa kutumia njia za
mitandao) kwenye Uwanja wa mkuu wa Taifa uliopo jijini Dar es Salaam
kuanzia Machi 3, 2015 hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi
hizo zitakapoondolewa.
Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu 60,000 na ndio uwanja wa kisasa zaidi uliojengwa na Serikali kwa ubia na watu wa Jamhuri ya China.Ni moja ya viwanja vinavyotumika kwa ajili ua mechi za ligi kuu na za kimataifa.
TFF , kwa kushirikiana na moja ya benki kuu nchini Tanzania (CRDB), iliamua kuanzisha mfumo wa kununua tiketi kwa mashabiki kwa njia ya mtandao ili kuepusha usumbufu kwa mashabiki wa soka na pia kuzuia tiketi feki au ulanguzi kutoka kwa wachuuzi wa kawaida.
Hata hivyo, zoezi hilo, ambalo lilianzishwa pia katika viwanja vingine tofauti ikiwa kama sehemu ya majaribio, lilipata baadhi ya dosari ndogondogo, kama vile changamoto za mtandao huku baadhi wakilalamika kuwa wanapata usumbufu wanaponunua tiketi ,wakati mwingine aidha kukoseana au kuchelewa kuleta majibu kama muamala umefanikiwa au la.
No comments:
Post a Comment