Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa linaitaka serikali ya Burundi na
wanasiasa wa upinzani, kuepuka matamshi yanayoweza kusababisha
machafuko nchini humo kuelekea ,wakati na baada ya Uchaguzi wa urais
mwezi Juni mwaka huu.
Wajumbe hao 15 wameongeza kuwa vitisho vinaweza kusababisha
hali kuwa mbaya hasa wakati huu ambapo tayari zaidi ya watu elfu nane
wamekimbilia nchini Rwanda kwa hofu ya kuzuka kwa machafuko machafuko.
Burundi pia imetakiwa kuhakikisha kuwa kuna mazingira mazuri ya uchaguzi huo kufanyika kwa njia ya amani, na zoezi hilo linakuwa huru na haki.
Siku ya Ijumaa, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya na kuzuia maandamano ya upinzani jijini Bujumbura kumshinikiza rais Piere Nkurunza kutowania urais kwa muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment