Monday, 11 May 2015

Liverpool hebu msikilizeni Louis Van Gaal ...

KOCHA Mkuu wa Manchester United, Louis van Gaal, amesema sasa anaweza kupata nguvu ya kutazama mechi za Liverpool tena akiwa na glasi ya mvinyo baada ya kushinda mabao 2-1 ugenini kwa Crystal Palace juzi Jumamosi.
Van Gaal alisema mechi hiyo ilikuwa muhimu kwao na kama wangefungwa au kutoka sare, basi asingekuwa na uthubutu wa kutazama mechi za Liverpool, mshindani mwenzake kwenye kusaka nafasi ya nne katika Ligi Kuu England.
Liverpool jana Jumapili jioni ilitarajia kumenyana na mabingwa Chelsea na Van Gaal alisema mechi hiyo haina tena presha kwake na anatazama huku akiwa na kinywaji mkononi.
Mabao ya Juan Mata na Marouane Fellaini yalitosha kuipa ushindi Man United na kuondoa presha ya kocha wake ambapo sasa anatakuwa anasaka ushindi wa mechi moja tu kati ya mbili kujihakikisha nafasi ya nne.
Kabla ya mechi ya jana ya Liverpool, Man United iliikua imeiacha timu hiyo kwa pointi saba, pengo ambalo linamfanya Mdachi huyo kuamini kwamba hawezi kufikiwa na Liverpool kwa mechi zilizobaki kama watashinda mechi moja kati ya mbili walizobakiza kwenye Ligi Kuu.
“Soka ni mchezo wa uchizi sana, hebu tazama vile tulivyocheza dhidi ya Chelsea, Everton na West Brom tulikuwa bora uwanjani tofauti na mechi hii ya Crystal Palace,” alisema
“Hii mechi tuliyocheza hovyo tumeshinda, zile tulizocheza vizuri
zote tumefungwa, ndivyo soka lilivyo.”

No comments:

Post a Comment