Raia wa Nepal wanaendelea kuwa na hofu baada ya nchi hiyo kupigwa kwa
mara nyingine na tetemeko la ardhi ikiwa ni siku kumi na saba tu, baada
ya tetemeko jingine kubwa kuipiga nchi hiyo na kuua zaidi ya watu elfu
nane.
Tetemeko hili jipya limesababisha vifo vya watu zaidi ya arobaini na vifo vingine kumi na saba kutokea kaskazini mwa India.
Hata hivyo kumekuwa na wasiwasi mkubwa wa idadi ya majeruhi wa janga hilo kuongezeka hapo baadaye.
Wanakijiji
wanaoishi karibu na eneo la maonesho ya hadhara Mashariki mwa mji wa
Kathmandu walishuhudia nyumba zao zikiporomoka kama mwamba milimani .
Watu
kadhaa waliopolewa kutoka katika matope yaliyokuwa yamewafunika kwenye
magofu ya zilizokuwa nyumba zao. Huko Kathmandu jengo la Bunge la nchi
hiyo lilionekana katika runinga likitikiswa kwa kasi kubwa huku majengo
ya serikali nchini India yalionekana kuharibiwa vibaya.
No comments:
Post a Comment