DARASANI-klasii


 TUTOKE VIPI ?DARASA LA TUTOKEVIPI?     na   TICHA SAM ...

1. MAANA NA UTOFAUTI KATI YA UKUAJI WA UCHUMI NA MAENDELEO YA KIUCHUMI

·       Ukuaji wa Uchumi: ni mabadiliko katika ukuaji kutoka kiwango cha awali kikilinganishwa na kiwango cha asasa. Tofauti kati ya kiwango cha ukuaji cha mwaka uliopita na ukuaji wa sasa ( Mwaka husika). Mfano mwaka 2005 – ukuaji ni 6% na mwaka 2006 ni 7%. Kilichoongezeka pale ndio ukuaji wenyewe katika asilimia. Ukuaji huu unakokotolewa kwa ukuaji katika kila sekta za kiuchumi na kwa maana hii basi ukuaji wa uchumi unahusika moja kwa moja na ukuaji wa sekta za kiuchumi. Mfano sekta ya kilimo, madini n.k

·       Maendeleo ya Kiuchumi: ni madiliko ya hali ya juu kiuchumi kutoka hali fulani ya kawaida kwenda hali nzuri zaidi.
·       Ukuaji wa Uchumi ni muhimu katika maendeleo ya uchumi japokuwa haujitoshelezi kusema kuwa nchi ina maendeleo ya kiuchumi. Hii ni kwa sababu kusema nchi ina maendeleo ya kiuchumi kuna mambo mengine ya kungalia kama ajira, kiasi cha umaskini na mambo mengine ya ustawi wa jamii.

·       Maendeleo ya kiuchumi ni ni muhimu na yanajitosheleza kusema kuwa nchi imeendelea. Maendeleo yanaangaliwa mbali na uchumi kuna masula ya kijamii, kitamaduni, na kiasiasa.




2. JE? UKUAJI WA UCHUMI UNAWEZA KUBADILISHA MAISHA YA MTANZANIA WA HALI YA CHINI MOJA KWA MOJA?
·       Mara nyingi wananchi wengi wamekuwa wakilalamikia uongozi wa nchi kuwa uchumi unakuwa lakini mwananchi wa kawaida hafaidiki.  Jambo hili limejitokeza na ukweli ni kwamba ukuaji wa uchumi wa Tanzania haujaweza kubadilisha maisha ya watanzania hasa walio wa chini.

·       Kama nilivyosema hapo awali kuwa ukuaji wa uchumi kama hautahusisha masula muhimu ya maisha ya watanzania kama ajira na masuala ya ustawi wa jamii bado mtanzania wa kawaida hataweza kufaidika.

·       Ukokotoaji wa ukuaji wa uchumi unahusisha sekta kama kilimo, ujenzi, madini n.k; hivyo basi kama fedha nyingi za nchi zilielekezwa katika sekta ya ujenzi wa barabara na majengo kwa kiasi kikubwa hivyo hivyo ukuaji huo utaonekana umeendelea vyema lakini kwa sababu ya sekta moja.

·       Je? Ni watu wote wanafanya kazi za ujenzi? Je Ustawi wa Jamii na ajira zitawafikia wananchi wote?
HITIMISHO: Ukuaji wa uchumi kama hautazingatia masuala mengine ya ustawi wa jamii n.k na kuhakikisha uhusishwaji na uboreshwaji wa sekta zote wakati wa utekelezaji wa mipango ya nchi basi kuna baadhi ya wananchi hawataona matunda ya nchi. Ukuaji wa Uchumi ni muhimu lakini haujitoshelezi kusema kuwa wananchi wote wamefaidika au nchi imeendelea..




                            UHURU WA KIFEDHA


Kupitia kuwa Afisa wa kampuni kubwa anayelipwa vizuri (Highly paid executive). Ukiwa mkurugenzi mkuu mtendaji wa TBL, CRDB, Cocacola, Vodacom etc mshahara wako ni milioni 20 au zaidi pamoja na marupurupu mengine ya kumwaga kila mwezi. Hivyo hawa mabosi tayari wana nafasi kubwa ya uhuru wa kifedha kama wataweka akiba na kuwekeza kwenye assets. Kama unavutiwa na njia hii jambo pekee ni kufanya bidii ya ‘kufufuka mtu and to ‘keep your nose clean’ throughout your career.
Na uwe tayari, sometime, kufanya kazi kwa miaka mingi sana ili kufika juu. Asilimia 10 ya matajiri wote duniani wanatoka kundi hili.
2. Kupitia kuwa mwanataaluma aliyebobea. Flying doctors, (Think about the Ben Carsons of this world), wanasheria wakuu, top accountants etc! Wanalipwa vizuri. Hapa inabidi uwe umeenda shule kweli kweli ili ufike huko. Kama hauko vizuri darasani, huwezi ku win kwa njia hii. 10% ya matajiri wote wanatoka hapa.
3. Watu wa mauzo au mameneja wa mauzo. Hawa hufika juu kama wako kwenye makampuni yenye kamisheni kwa wale wanaofanya vizuri! Huwa hakuna kikomo cha idadi ya watu unaoweza kuwauzia kama una ujuzi wa kutosha wa bidhaa unayoiuza, mipango mizuri inayotekelezeka na bidii ya hali ya juu. 5% ya matajiri wote hutokea kundi hili.
4. Watu wenye vipaji maalum; wanamichezo nyota, wanamuziki maarufu (The Diamonds of this world) wachekeshaji kama akina Masanja, Joti, nje akina Jerry Seinfeld, Chris Rock, Chris Tucker etc, waandishi mashuhuri akina John Grisham, Paolo Coelho, kina Shigongo hapa nyumbani n.k. Hawa huwa ni 1% tu ya matajiri wote ulimwenguni. Watu wengi hudhani hawa huwa ni wengi kwa sababu ya kufahamika kwao kupitia vyombo vya habari!
Sasa, guess what? Unajua tumebakisha asilimia ngapi?
74%. Yes 74%!. Asilimia 74 ya matajiri wote duniani ni WAJASIRIAMALI. Kuanzia kuuza mayai ya kanga, kufuga sungura, kuuza mazao, maduka, migahawa, elimu, internet biz, network marketing etc. Wote huo ni ujasiriamali. 
Watu wengi wana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kwenye ujasiriamali kuliko hayo maeneo mengine manne.
Ndiyo maana ninahubiri ujasiriamali! Najua ninaweza kuwasaidia watu wengi kupitia njia hii kuliko kupitia kuwa highly paid execs or professionals. But still jambo la muhimu sana kwako ni kufuata kitu ambacho roho yako inapenda.
Swali muhimu ni wewe unachagua mlango gani katika milango hii mitano?
Japo kuwa inawezekana kuwa na mlango zaidi ya mmoja, chagua kwanza mlango mmoja halafu fanya kweli yaani simama imara halafu mengine yanawezafuata!

            

              UGONJWA WA KISUKARI  


Leo tunaendelea kuchambua ugonjwa wa kisukari na tutaanza na madhara kwa wajawazito kisha tutatoa ushauri: Endelea.

Masharti ya kurekebisha mpangilio wa chakula na kuacha au kupunguza kula vyakula vyenye sukari na mafuta, kufanya mazoezi na pia kutumia vidonge yanafaa kuzingatiwa kama tulivyoeleza wiki iliyopita.

Wajawazito nao hupata kisukari kitaalam hujulikana kama Gestational Diabetes. Hali hiyo husababishwa na mahitaji ya Insulin kuongezeka kipindi cha ujauzito hasa wale wanawake wanene.

 Hata hivyo, hali hiyo huisha baada ya mjamzito kujifungua. Lakini tafiti zinaonyesha kuwa wanawake huwa katika hatari kubwa ya kupata kisukari kadiri umri unavyozidi kuongezeka.
USHAURI
Pia njia za kutibu ugonjwa wa sukari hutolewa hospitalini, na hayo ni matibabu maalumu ya aina ya Hyperosmolar non-ketotic .
Mkazo huwekwa katika kusahihisha upungufu wa maji mwilini ambapo mgonjwa hupewa kati ya lita 8 hadi 10 za maji aina ya Normal saline. Iwapo kuna ugumu katika kusahihisha kiwango cha sukari mwilini kwa kutumia dawa za kunywa, Insulin inaweza kutolewa.

Matibabu mengine maalumu ni ya kutibu Diabetic Ketoacidosis (DKA). Kama ilivyo kwa Hyperosmolar non-ketotic coma, matibabu ya DKA nayo hutolewa hospitali chini ya uangalizi maalumu wa madaktari.

Hii ni hali ya hatari, ambapo isipotibiwa kwa umakini, inaweza kumuua mgonjwa. Jambo la muhimu katika matibabu haya ni kusahihisha upungufu wa maji mwilini, kusahihisha kiwango cha Potassium katika damu na kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu kwa kutumia Insulin.

Sukari isipodhibitiwa ipasavyo mwilini  inaweza kuharibu ufanisi wa figo, mgonjwa hulazimika kutolewa figo, sukari ikiwa juu mgonjwa akipata kidonda si rahisi kupona na kusababisha kukatwa kwa kiungo kama mguu au vidole vya mguu kwa sababu mara nyingi vidonda hivi huwa kwenye miguu.

Vilevile, anasema mgonjwa hupoteza uwezo wa kuona na kusikia, hupoteza nguvu za kiume na mara nyingi husababisha kifo.

Kisukarii kinaweza kudhibitiwa kwa kufuata masharti ipasavyo, kwa wagonjwa wa kisukari ni muhimu kuzingatia matumizi ya sindano ya Insulin au vidonge kama daktari alivyoelekeza.

No comments:

Post a Comment