TEKNOLOJANJA

 TUTOKE VIPI ?


ATM ZA MAJI ZA GEGNGESHA KENYA ....


Maji ya ATM nchini Kenya
Wakazi wa kitongoji duni cha Mathare katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, sasa wanaweza kupata maji safi ya kunywa na kwa matumizi mengine.
Mpango unaoungwa mkono na serikali umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi unaowawezesha watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda kununua maji kwa kutumia kadi.
Vituo vya kuuza maji vimebuniwa kote katika sehemu za mabanda ambapo wenyeji hutumia kadi zilizo na pesa kununua maji safi na kwa bei nafuu.


null
Maji ya ATM nchini Kenya
Wenyeji wa mitaa ya mabanda nchini Kenya wamekuwa na tatizo la kupata maji safi ambapo hulazimika kununua maji kwa bei ghali kutoka kwa wauzaji au kutoka kwa magenge ambayo hudhibiti na kuuza maji hayo kwa kuyachuuza.
Mradi kama huo umefaulu katika baadhi ya maeneo ya vijijini nchini Kenya, lakini hii ni mara ya kwanza kuzinduliwa katika mji huo mkuu.


null
Maji ya ATM nchini Kenya
Vituo hivyo vya kutoa huduma hiyo ya maji vimefanikiwa kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya mitaa nchini Kenya na kampuni ya maji ya Grundfos ya Denmark.
Kampuni ya kusimamia huduma ya usambazaji maji, ina mikakati ya kuhakikisha kuwa huduma hii walioianzisha itasambazwa kote katika mji mkuu wa Nairobi na kwengineko nchini humo.


null
Maji ya ATM nchini Kenya
Huku hilo likianzishwa wakaazi wa mitaa kadhaa mjini Nairobi bado wanalalamikia ukosefu wa maji.

 
                ROBOTI IMEFIKA NA KUTUA KWENYE KIMONDO ><><><><

              

Baada ya safari ya miaka kumi katika anga za juu, chombo cha anga za mbali cha Ulaya kimevuka kilomita chache za mwisho kutoka ardhini kutekeleza kile kitakachokuwa kifaa cha kwanza kuwahi kutengenezwa na binadamu kutua kwenye kimondo.

Roboti hiyo iliyotengezwa Ulaya kwa jina Philae, imefanikiwa kutua katika kimondo likiwa ni jambo la kihistoria kuwahi kushuhudiwa. 

Aidha roboti hiyo ilitua katika Kimondo kinachojulikana kama 67P/Churyumov-Gerasimenko saa kumi jioni saa za Ulaya.

Kulikuwa na vifijo na nderemo pamoja na wanasayansi kupigana pambaja katika chumba ambako shughuli hiyo ilikuwa inadhibitiwa mjini Darmtadt, Ujerumani baada ya ishara kuonyesha kuwa roboti hiyo ilikuwa imetua kwenye kimondo. 

Ishara ya kuonyesha kuwa roboti hiyo ilifanikiwa kutua ulikuwa mwanga kutoka kwenye roboti hiyo. 

"Hii ni hatua kubwa sana katika historia ya binadamu kulingana na wanasayansi hao




UTAFITI .....><><><>< UGUNDUZI WA MASHINE YENYE UWEZO WA KUFIKIRI KISHINDO ><>>>


                           

Profesa Stephen Hawking, mmoja wa wanasayansi mahiri nchini Uingereza, amesema juhudi za kutengeneza mashine inayofikiria inatishia uwepo wa binadamu.

Ameiambia BBC:"Kutengenezwa kwa mashine yenye uwezo wa kufikiria inaashiria maangamizi ya binadamu."

Onyo la Profesa Hawking limekuja kutokana na kuimarishwa kwa teknolojia anayotumia katika mawasiliano, ambayo inahusisha msingi wa Akili Bandia(Artificial Intelligence, AI).
Lakini wengine hawana upinzani sana na matarajio ya teknolojia hiyo ya AI.

Mwanasayansi huyo wa nadharia ya fizikia, ambaye anaumwa ugonjwa wa mishipa ya fahamu (ALS), anatumia mfumo mpya uliotengenezwa na kampuni ya Intel kuzungumza.



 
Wanasayansi wakifuatilia kifaa chenye muundo wa kufikiri kama binadamu
Wataalam wa mashine za kujifunza kutoka kampuni ya Uingereza ya Swiftkey pia walihusika katika kunda mashine hiyo. Teknolojia yao, tayari inatumika kama mfumo wa smartphone, unajifunza namna profesa Hawking anavyofikiria na kupendekeza maneno ambayo huenda angetaka kuyatumia baadaye.

Profesa Hawking amesema miundo duni ya akili bandia (AI) ambayo imeboreshwa mpaka sasa imethibitisha kuwa na manufaa sana, lakini ana wasiwasi wa madhara yanayotokana na kuunda kitu chenye uwezo sawa na binadamu au kupita. "Mashine hiyo inaweza kujiwasha na kujizima na kujibadili yenyewe katika kiwango kisichomithilika," amesema.

Cleverbot ni kifaa(software) ambacho kimeundwa kuwasiliana kama binadamu anavyofanya "binadamu ambao wana ukomo wa kufikiri kutokana na mabadiliko ya taratibu ya kibaolojia, hawawezi kushindana na mashine hii, na watapitwa kwa mbali."




WAZUNGU WAMETENGENEZA MBEGU ZA KIUME !! 

Seli za mbegu za kiume zimetengezwa katika maabara kwa mara ya kwanza na hivyobasi kuwapa matumaini wanaume wasio na uwezo wa kupata watoto.

Kampuni moja nchini Ufaransa imedai kwamba imefanikiwa kubadilisha vipande tofauti vya maumbile hadi kupata mbegu za kiume zinazoweza kutoa mtoto kwa mara ya kwanza.

 
Iwapo uzinduzi huo utathibitishwa ,huenda ukabadilisha maisha ya wanaume wengi duniani ambao hawawezi kutoa mbegu za kiume.

Maabara ya Kallistem,kituo cha kibinafsi cha utafiti kilichopo mjini Lyon kimesema kuwa kitaweza kufanya majaribio katika kipindi cha miaka miwili.
Iwapo uzinduzi huo utaingia sokoni,kampuni hiyo inataraji kuwatibu watu 50,000 kila mwaka soko ambalo linaweza kuwa na thamani ya pauni bilioni 1.7 .

Hatahivyo matokeo ya utafiti huo hayajachapishwa ama hata kuthibitishwa huku wataalam wa Uingereza wakichukulia uvumbuzi huo kama uvumi tu.

Kalliste imesema kuwa imefanikiwa kubadilisha seli za kawaida katika mbegu za kiume hadi mbegu za kiume zilizokomaa.



Bugatti Grand Sport Vitesse 1 of 1 2



THE BUGATTI VEYRON 2013

Natoa heshima yangu kwa BUGATTI engineers na kwa gari lenyewe 2014 BUGATTI VEYRON …



THE BUGATTI VEYRON 2013 … invention a kipekee ya gari duniani zitaundwa mia tatu tu duniani pote .
Natoa heshima yangu kwa BUGATTI engineers na kwa gari lenyewe 2013 BUGATTI VEYRON … RESPECT 

Dr . Franz – Josef Peafgen  PRESIDANT BUGATTI AUTOMOTIVE
Engine Designer : ANDREA SCHAFER aliziunganisha injini mbili za V8 ili kupata injini moja ya BUGATTI na akaiita W16 .

Inamchukua mtengenezaji masaa kumi na tano (15 hrs) kutengeza rejeta moja ya bugati ,.. na kila gari moja (yaani BUGATTI  moja) ina rejeta kumi .
Unapoiwasha nakuondoka inauwezo wa kumaliza top speed ya 250 miles per hour kwa sekunde chini ya 17   .
Ni gari pekee duniani ambayo ilitengenezwa kwa kutumia technolojia ya anga ( erospace technology ) kwa kutumia madini ya solid titanium (hutumika kwa matumizi ya kuunda ndege ) alumini na inaunganishwa na bolt kumi na nne tu kati kati kuunganisaha sehemu ya nyuma ilipo injini na mbele  .. gari hii haina chansesi  .

Inachukua muda wa wiki moja nzima kuungasha tena kwa mikono ya binadamu (hand made) injini moja ya BUGATTI .

Hii ndio gari pekee inayokwenda mbio kuliko ndege aina ya JET inaporuka , kama wasingetumia solid titanium joto la HP 1001(HP ni hos pawa) lingewza kuleta joto kwa familia mia moja kipindi cha baridi kali .
BUGATTI ina injini mbili na gia box mbili kwa pamoja maana yake ni kua gari hii inaingiza gia ya kwanza na yapili iko mgongoni saa hiyo hiyo inasubiri ku take off yaani BUGATTI inaingiza gia mbili kwa mara moja .
BUGATI TERO ni kaka wa BUGATTI VEYRON na zilianza kutengenezwa mwaka 1909 mpaka 1947 na mwaka 1998 VW Volkswagen ya ujerumani ilinunua BUGATTI TERO na miaka miwili baadae wakaamua kutengeneza gari yenye mbio na uwezo kuliko zote DUNIANI .

Hii gari tairi yake ni pana inch. 14 mara mbili ya tairi ya gari ya kawaida na imepimwa na kuundwa na wataalam wanaotengeneza tairi za ndege kubwa duniani inapimwa uwezo wake kwa pico seconds ni mara bilioni 1000 ya sekunde moja . UPO ?

BUGATTI UKIWA TOP SPEED YAANI UMEFUTA UKAGUSA  ..BREKI .. INASIMAMA CHINI YA SEKUNDE KUMI .

Bugatti ina mifumo miwili ya breki , breki ya kimakenika na breki ya upepo huu wa kawaida unaotupiga tukiwa tunatembea bara barani .

MATHIAS TAPPENBECK na wenzake walitumia miaka mine ku design tank ya mafuta ya hii gari ambayo itaskuma mafuta kwa haraka mara 8 zaidi ya gari ya kawaida .

Tairi nne za BUGATTI zina gharimu paundi elfu kumi na moja hii ni sawa sawa na shilingi za Tanzania milioni ishirini na nane na laki sita 28,600,000/= na tairi jizi hutumika kwa miezi sita tu kabla ya kuzibadilisha kwa usalama, (Samahani ki ukeli gari yako ulinunua sh. Ngapi WEMA ?

BUGATTI inaunganishwa vipande 2500 kukamilisha uundwaji wake … ni gari ya maajabu .
HEGAMAN EROSPACE .
VW .                                                 I RESPECT .. BUGATTI NDEGE YA CHINI





                                   hiyo nyeupe ni meli ya OASIS

 


               

Aje Aje... mazee ! ts another day man ... mungu ni mwema stil ...

Check this >>





OASIS OF THE SEA …… FARAJA ILOUMBWA NA MWANADAMU KWA MIKONO
MY RESPECT TO OASIS CRUIZ SHIP … NGOROMIKO 


Unaikumbuka TITANIC ?  Kuusema ukweli wengi tuliijua baada ya kuimbwa na Celine .
Tukajua ile ndio ilikua meli kubwa kuluko duniani … ila hatukujua ilikua ni kwa wakati ule tu .

OASIS OF THE SEA
Meli ya starehe yenye ukubwa mara tano ya TITANIC .

Inauwezo wa kubeba abilria 5400 na inawafanyakazi 2200 wa melini tu .

Bata linahusisha mambo mengi , kwenye OASIS yamooo! , ina swimming pools 21 

Ina restaurant 24, inatoleo lake yenyewe la eneo la new York city laitwa central park 

Kila abiria mmoja kwenye OASIS  anahudumiwa kama yupo peke yake na abiria wapo 5400 kwenye meli moja … ikiwa unataka eneo kwa shughuli kama hii utahitaji STUDIUM mbili ili kuwapa naafaas mtu mmoja mmoja ila kwenye meli hii imewezekana 



CAPTAIN: WILLIAM WRITS


My respect; He is the captain to OASIS 

GHARAMA ZA KUUNDA OASIS


Gharama ya kuunda hii meli kubwa zaidi duniani ni dola za mmarekani billion moja na milioni mia nne +.

(hivi umenielewa ??) 1.4 BILLION $ kwa pesa hii Magufuli angejenga bara bara mpaka kwenye kila geti au chumba nchi nzima , wananchi wa lowassa Monduli wangekua ndio matajiri zaidi kuliko mtu yeyote Tanzania and may be AFRICA , na kama wangepewa NASA wange launch (yaani kurusha ) space ship (yaani chombo cha anga kinachosafiri sayari zingine huko) MARA 3 .



MACHINARY (INJINI ZA HII MELI mwanangu ) .

OASIS OF THE SEA ndio yaitwa hivyo ina injini tatu
Kila injini inuwezo wa kuzunguka 360* (yaani kuzunguka moja kwa moja kwa ubavu wa upande wowote ) .

Ina uwezo wa HP 2700 (HP maana yake ni hospawa ) yaani nguvu ya injini malory kama semi trela yana HP 1000 – 1000+ na gari yenye mbio kuliko zote duniani in HP 1001 INJINI MOJA YA OASIS INA HP 27000 NA ZIPO TATU .
OASIS ina restaurant 27 na ina baa ya lifti (elevator bar )

Ina SWIMMING POOL 21
Meli pana zaidi ya kitalii upana wake ni mita 38 OASIS ina mita 47
Ina kumbi kadhaa za kula raha moja wapo ni AQA THEATER wenye uwezo wa kubeba watu 600 kwa wakati mmoja 

OASIS OF THE SEA …. KAMA WENZETU WAMEFIKA HAPA … sisi tupo wapi ????? kijana its time
Tutaendelea ……













Viatu hivi vina uwezo wa kujifunga kama vyenyewe
Ni miaka 26 tangu tuone viatu vikijifunga kamba zenyewe kama ilivyokuwa kwenye matangazo ya biashara ya viatu vya Nike vyake Marty McFly vikijifunga miaka hio. hio


Hilo lilikuwa tu tangazo la bishara zamani sana lakini kuna mtu ambaye aliwaza hivyo miaka hiyo na kusema atakuja kuzindua viatu vyenye uwezo wa kujifunga kamba. Na kwake ndoto hio imetimia.
Wahandisi nchini Ujerumani wamebuni viatu ambavyo vina uwezo wa kujifunga kamba.


Walifanikiwa kufanya hivyo kwa kuweka 'cherger'mfano kama ile ya simu kwenye viatu hivyo ambavyo vinatumia kawi kujionea wenyewe itakavyokuwa kwenye miguu tofauti.
Pindi unapovaa kiatu hicho, sensa ya kiatu inakiambia kwamba mguu uko sawasawa na kuchochea kawi kwenye kiatu kile kuamrisha kamba kujifunga zenyewe.
Wakati unataka kuvua viatu utahitajika kubonyeza au kugonga wayo wa kiatu kile mara mbili na vile vile kuna miale inayoamrisha kamba za viatu vile kujifungua kwa kuzilegeza kamba.
Wanasema kiatu hicho hakihitaji kuwekwa kwenye charger au kubadilisha betri kwa sababu kawi inatokana na hatua za kuukanyaga mguu chini kwa mvaaji au anapotembea zile hatua ndizo zinakipatia kiatu nguvu au kawi.

Mmoja wa wahandisi waliokitengeza kiatu hicho, anasema kwamba kiatu hicho kitawasaidia watu wengi.
Miongoni mwa watakaofaidi ni watu wanaokumbwa na ulemavu wa miguu au wenye matatizo ya kutembea lakini pia vinaweza kuwasaidia watoto au kwa wanaotaka tu kubadili mfumo wao wa maisha.

Saa moja ya kutumia viatu hivyo inatosha kuweza kurejesha kawi ya kufunga kamba.
Bwana Ylli na kikundi cha wahandiisi wengine wanashughulikia kifaa kingine ambacho kitawezesha viatu kumuonyesha mvaaji mwelekeo anakokwenda.





BOSS WA MICHEPUKO <>  <> UGUNDUZI WA MICHEPUKO POLICE 


Kampuni moja ya kimarekani imegundua kifaa kinachoitwa "semenspy" kitakachokuwa na uwezo wa kutambua iwapo mwenza katika mahusiano amechepuka....mwenye mashaka na mwenzie atahitjika kuchukuwa nguo za ndani za mwenzie na kutumia kifaa hicho...majibu utayapata muda huo huo



Choo cha Kukalia Nyumba nyingi mijini na ofisi mbalimbali zinazojengwa hivi sasa, huwekewa vyoo vya kukaa. Hata zile za zamani zinakarabatiwa na kubadilishwa kwa kuwekewa hivi ambavyo vinaonekana vya ‘kisasa’.
Mgunduzi wa vyoo vya aina hii, Thomas Crapper anasema kwa mtazamo wake aliona kukaa wakati wa kujisaidia ni utambulisho wa ustaarabu na maendeleo.
Hata hivyo, madaktari wanapingana naye wakisema kujisaidia katika vyoo vya kukaa kuna madhara kiafya kwa kuwa mkao huo unaweza kuleta matokeo mbalimbali ndani ya mwili.
Utafiti uliofanywa na mtandao wa ‘naturesplatform’ umegundua kuwa matumizi ya choo cha kukaa huweza kusababisha matatizo mbalimbali ikiwemo kansa ya utumbo mkubwa.
Mtaalamu wetu wa afya , Samwel Shita anasema, madhara ya vyoo vya kukaa ni makubwa kwani wakati mwingine yanaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa kutokana na haja kubwa kubaki kwa muda mrefu katika utumbo huo.
Shita anasema mtu anapojisaidia haja kubwa katika choo cha kuchuchumaa, kinasaidia haja yote kutoka kwa sababu ya msukumo unaosababishwa na mkao huo.
“Unapokaa unakuwa umekaa katika choo mwili unakuwa umelegea, hivyo inabidi utumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tofauti na unapochuchumaa,” anasema Shita na kuongeza:
“Matatizo huanza hapo, unapojisaidia ukiwa umekaa na kulazimisha kujikamua unaweza kusababisha vimishipa vidogo katika utumbo mpana sehemu ya haja kubwa ya ndani na ya nje kuvimba na maumivu makali husababishwa na ugonjwa unaojulikana kama ‘hemorrhoid,” anasema.
Anasema ‘hemorrhoid’ ni ugonjwa ambao pia huitwa bawasiri. Mgonjwa hupata uvimbe katika njia ya haja kubwa na hivyo kupata maumivu wakati wa kujisaidia na haja yake mara nyingine huambatana na damu.
Aidha, anasema vyoo hivi pia vinaweza kuwa chanzo cha magonjwa yanayotokana na shambukizi katika utumbo mpana, kitaalamu ‘Inflammatory Bowel Disease’.
“Kila binadamu anapaswa kujisaidia na kuhakikisha haja yote imetoka na kwisha kabisa, inapobakia inaweza kusababisha maambukizi katika utumbo mpana kwa kuwa ule ni uchafu wenye mchanganyiko wa vitu vingi,” anasema Shita.
“Haja kubwa inapokuwa tayari imeshajitengeneza inapaswa kutoka yote, kama itabaki kipindi kirefu inaweza pia kuleta uambukizi katika utumbo mkubwa na hata katika kidole tumbo,” anasema Shita.
“Uchafu huu si tu unaweza kusababisha maambukizi, lakini pia unaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa. Wote tunajua kuwa mkusanyiko wa sumu mbalimbali mwilini unakuweka katika hatari ya kupata saratani, hivyo tatizo hili lisipotafutiwa ufumbuzi mapema linaweza kufikia huku,” anasema Shita.
Daktari Berko Sikirov kutoka Misri ambaye alifanyia utafiti matumizi ya vyoo vya kukaa anasema kuwa iwapo mtu ana tatizo la vivimbe vya ‘hemorrhoid’ linaweza kumalizika iwapo ataacha kutumia vyoo vya kukaa.
Hata hivyo, anasisitiza kuwa tatizo hili linaweza kwisha kama litakuwa katika hatua za awali. Kwa wenye tatizo lililokomaa watalazimika kufuata matibabu kulingana na ukubwa wake.
Dk Sikirov anaongeza kuwa mbali na kupata vivimbe, pia mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutokupata choo kwa muda mrefu.
Anabainisha kuwa kitendo cha haja kutoka kidogo na nyingine kubakia husababisha kuganda katika ukuta wa utumbo na zoezi hilo huendelea mpaka kuwa tatizo sugu.
“Haja kubwa huganda katika kuta za utumbo, hali hii huifanya haja izunguke kwa muda mrefu na ndiyo tatizo hili huanzia hapa,” anasema na kuongeza:
“Unapojisaidia ukiwa umekaa, ile njia ya haja kubwa huwa kama imejifunga, inabidi utumie nguvu nyingi sasa ukiwa na tatizo hili la kukosa haja kubwa huifanya itoke kwa uchache zaidi,” anasema Dk Sikirov.

Aidha, anasema kupata haja kubwa mara kwa mara ni muhimu kwa kuwa usipoitoa maana yake inazungusha sumu katika damu jambo ambalo ni hatari kwa afya.
Anaongeza kuwa kutopata haja kubwa ni kichocheo chenye uwezo mkubwa wa kusababisha saratani ya utumbo mkubwa na uambukizi katika kidole tumbo.
Tafsiri ya kitabibu inasema hali ya kukosa haja kubwa ni pale mtu anaposhindwa kuipata angalau mara tatu kwa wiki. Hata hivyo, ili ujue afya yako ni njema unapaswa kuwa unapata haja kubwa angalau mara moja kila siku.
Daktari Denis Burkitt aliwahi kuandika kitabu cha maelekezo ya chakula ili kuepuka ugonjwa wa saratani. Katika kitabu hicho alieleza namna ambavyo watu wanaweza kujikinga na saratani za aina mbalimbali.
Akizungumzia saratani ya utumbo mpana pamoja na kuelezea vyakula na aina ya maisha, pia aliwaasa watu kutumia choo cha kukaa ili kujiepusha na tatizo hilo.
Anaeleza kuwa kwa Marekani pekee, watu zaidi ya 150,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa.
Mtaalamu wa Ngozi katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Kisali Pallangyo anasema matumizi ya vyoo hivyo yanaweza kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa ya ngozi. Profesa Pallangyo anasema ni rahisi kuambukizwa magonjwa ya ngono na ngozi kwa urahisi pale unapotumia vyoo vya kukaa tofauti na vile vya kuchuchumaa.
Aidha, anayataja magonjwa yanayoweza kuwambukizwa kwa kutumia vyoo vya kukaa kuwa ni kaswende, harara, mba, kisonono, upele na mengine.
“Mtu mwenye magonjwa ya ngozi au ya ngono, anaweza kuyaacha katika ‘sink’ anapolikalia, hivyo ni rahisi kwa mtu mwingine ‘kuyachukua’ mara atakapokaa wakati wa kujisaidia,” anasema Prof Pallangyo.
Anasema vyoo hivi ni hatari kwa afya hasa pale vinapotumika katika jumuiya na kuongeza kuwa ni bora kutumia vile vya kukaa ili kujikinga na magonjwa. 



SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO, 2015
 
                                                                 UTANGULIZI

Sheria hii ya Makosa ya Jinai kupitia Mtandao, 2015 ina mapungufu mengi. Mapungufu hayo yamebainika kuwa, kama sheria ikipita yanaweza kuifanya nchi ikawa ni kati nchi adui za matumizi ya mtandao wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano duniani.
Watanzania wote wanatakiwa kufahamu kuwa muswada ukipita utatumika nchini kote yani Tanzania Bara na Visiwani.

Watanzania walio wengi hawafahamu Sheria hii inawahusu kwa namna gani; lakini kwa lugha rahisi ni kuwa itamuathiri mtu yeyote anayeweza tumia Mtandao wa Intaneti kwa kutimia kifaa chochote iwe kompyuta kubwa au vifaa vyenye uwezo wa kufanya kazi kama kompyuta kama Simu za mikononi, saa, televisheni na vifaa vingine vinavyoendana na hivyo.
Malengo ya Sheria hii ni kuainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
Matumizi ya mitandao yote mikubwa kama Twitter, Instagram, Facebook, Barua pepe, WhatsApp, blogu na data zote zilizo katika kifaa chochote cha kielektroniki yanaathiriwa kwa kiwango kikubwa na Muswada huu.

UCHAMBUZI

Kifungu cha 7
(1-3): Haibainisha ni aina gani za data ambazo haziruhusiwi kuguswa/kufutwa au zikiguswa/futwa ni kosa la jinai.

7(1g): Kipengele hiki katika kifungu hiki kinarudiwa mara kadhaa katika (Vifungu vya 32-35). Badala ya vifungu vya mbele kurejea kifungu hiki, watunga sheria wameiacha kifungu hiki kikiwa hakieleweki hadi mtu asome vifungu vya mbele.
Je mtu aliyeidhinishwa katika ibara na kipengele hiki ni nani?
Kifungu cha 8:
Muswada huu haujaweka bayana iwapo nyaraka za siri zinaweza kuwekwa wazi katika mtandao kama zina maslahi ya nchi au wananchi mf. Matumizi mabovu ya pesa za umma

Kifungu cha 14:
Neno pornografia halijapewa maana na hivyo jambo lolote lenye mwonekano wa kiasherati (sexually vulgar) linaweza kutafsiriwa kama pornografia na kumuingiza muhusika matatizoni.

Ponografia ya mtandao isikatazwe kabisa ila inatakiwa kuweka ulinzi thabiti wa kuhakikisha watoto hawawezi kufungua mitandao ya aina hiyo.
Ponografia zote ni chafu lakini sio chafu zote ni ponorafia. Hivyo kutokana na kuwa sheria hii inasema ponografia zote ni chafu hii itasababisha kila mtu ahukumiwe chini ya kifungu B.
Uchafu na Ponografia viwe vipengele viwili tofauti.
Kifungu cha 15:
Suala la kujifanya mtu mwingine kwenye mtandao, linaweza kuleta utata kwani kuna baadhi ya mitandao ambapo watumiaji hutumia majina ambayo sio ya kwao. Itakuwaje watu kwa madhumuni mabaya wakitafuta mtu mwenye jina kama hilo na kumshtaki mtumiaji wa mtandao?

Je, mtu kujifanya mtu mwingine inahusisha mtu kutumia jina lisilo lake hata kama hajajifanya mtu mwingine? Ni vema suala hili likafafanuliwa kisheria kwakuwa ni suala muhimu lakini wachache wataelewa manaa yake.
Kifungu cha 16:
Ni nani ana mamlaka ya kubainisha kuwa jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la UKWELI, UONGO au UPOTOSHAJI? Ni wazi kuwa mamlaka husika inaweza tumia hili kama mtego kwa manufaa yao.

Kipengele hiki kama vingine kimeambatanisha muda usiopungua bila kusema muda usiozidi. Hivyo mtuhumiwa anaweza kufungwa hata kifungo cha maisha kutokana na mamlaka ya mahakama.
Watu binafsi wanaweza kutumia vibaya kifungu hiki kuzuia uhuru wa maoni kwa kuwaburuza watumiaji wa mtandao mahakamani kila kukicha na kuwapotezea muda wahusika ambao wanaweza kubainika mwishoni kuwa walionewa.
Kifungu cha 20:
Katika mawasililano ya mtandao kama ilivyo mawasiliano mengine kuna ujumbe ambao mtu hawezi kuacha kuupata

Mfano kutembea barabarani na kuona bango la matangazo, au kuwa ndani ya daladala iliyowasha redio.
Vivyo hivyo katika mtandao sio kila ujumbe anaopokea mpokeaji ameuomba na hivyo kifungu hiki kinafanya kila mtu atakayepokea ujumbe bila ridhaa yake kuwa amefanya kosa la jinai.
Kifungu cha 21(1):
Tafsiri za Kiswahili na kiingereza zipo tofauti kabisa.

Ya Kiswahili inamlenga Mtoa Huduma na huku ya kingereza inamlenga mtu yeyote anayetumia mtandao.
Ya Kiswahili inamlazimu mtoa huduma kumtaja mhusika aliyeweka ujumbe na pia kumuadhibu mtoa huduma huku ya kiingereza inazungumzia kuhusu tafiti kwa ujumla.
Ya kiingereza ni nzuri lakini ya Kiswahili imepotoshwa na inavunja uhuru wa mawasiliano.
MUHIMU:
Hakuna kinga yoyote kwa mtoa taarifa (source) kwa mujibu wa ibara hii.

Kifungu cha 22:
Je, nani ana mamlaka ya kuamua kuwa ujumbe kwenye mtandao unatolewa au kuboreshwa kwa kusudi au bila kusudi.

Itambulike kuwa ujumbe wa kwenye mtandao huboreshwa (edit) au kufutwa wakati wowote muhusika anapoona inafaa mf. WhatsApp status, Facebook status nk.
Kifungu cha 23:
Unyayasaji wa kupitia mtandao (cyber bullying) haujapewa maana.

Sheria inatakiwa kuweka bayana maudhi ya kihisia ni nini.
Kwani mtu yeyote atakayeudhiwa ‘kihisia’ au kudai kuwa hisia zake zimeudhiwa anaweza kushtaki. Sio kila linalosababisha maudhi ya kihisia ni unyanyasaji
Kifungu cha 27:
Ni nani anaamua kitendo fulani ni kula njama? Mazungumzo ya kawaida na maamuzi ya kukubalika na upande mmoja yanaweza kutafsiriwa kama kula njama na watu wa upande mwingine.

Kifungu cha 31 (3a):
Sheria ya kiingereza inasema ‘as soon as practicable’ lakini ya Kiswahili inasema wakati wa upekuzi na ukamataji wa mali. Hizi zina maana tofauti.

Ibara hii inawapa mamlaka Wakuu wa Vituo vya Polisi kufanya upekuzi na kuchukua mali(za kielektroniki) na taarifa binafsi za raia bila amri ya Mahakama.
Kifungu cha 32-35
Ibara hizi zinamlazimisha mtoa huduma kutoa data za wateja wake kwa Mkuu wa kituo cha Polisi bila kibali cha Mahakama. Wakuu wa Vituo vya Polisi wamepewa nguvu sana katika sheria hii! Mahakama ipewe mamlaka haya na si Polisi, na ifanyike hivi baada ya kujiridhisha kuwa mwananchi anatakiwa kufanyiwa upekuzi, kuchukuliwa data zake au za wateja wake n.k

Kifungu cha 39-45
Watoa huduma na wahifadhi tovuti wanalindwa na ibara hizi lakini kwa masharti.

Katika ibara ya 39, Waziri anapewa mamlaka ya kuamua kipi ni kosa na kipi si kosa. Anapewa mamlaka ya kusimamisha na kusitisha huduma, kuondoa taarifa juu ya kitendo husika (mfano kulazimisha kuondoa mijadala yote ya ufisadi flani kama yeye ataona kwa mamlaka yake kuwa haufai kujadiliwa).
Muswada huu vifungu vya 31-38 na vifungu vya 39-46 zinakinzana kwani kwa wakati mmoja mtoa huduma anaweza akawa ameona jambo ameshalitoa na anajiandaa kuitaarifu mamlaka husika huku mamlaka husika (Askari Polisi) ikiwa na uwezo wa kwenda kuchukua vifaa na data za mtoa huduma.
Mamlaka ya Polisi imepewa kinga kubwa ambayo haiingiliani na sheria yoyote ile.

Baadhi ya Vipengele vya sheria hii ya mtandao
Kutoa taarifa za Uongo
16.- Mtu yeyote anayetoa taarifa, data au maelezo kwa njia ya picha, maandishi, alama au aina nyingine yoyote taarifa, data, kwenye m fumo wa kompyuta, endapo au maelezo hayo ni ya uongo, yanapotosha au yasiyo sahihi, atakuwa ametenda kosa, na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia adhabu ya kifungo kisichopungua miezi sita au vyote.

Kwa kiingereza:
Publication of false information
16.- Any person who publishes information, data or facts presented in a picture, text, symbol or any other form in a computer system where such information, data or fact is false, desceptive, misleading or inaccurate commits an offence, and shall on conviction be liable to a fine not less than three million shillings or to imprisonment for a term not less than six months or to both.

21.-(1) Mtoa huduma anayepokea amri kuhusiana na upelelezi wa kijinai, inayohitaji usiri, hatatoa taarifa yoyote iliyopo kwenye amri hiyo isivyo halali na makusudi.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote.
Soma pia kuhusiana na watoa huduma:

Disclosure and collection of traffic data
34.-(1) where there is a reasonable ground that a computer data is required for the purpose of investigation, a police officer in charge of a police station or a law enforcement officer of a similar rank may issue an order to any person in possession of the data for-
(a) disclosure, collection or recording of the traffic data associated with a specified communication during a specified period; or
(b) permitting and assisting the law enforcement officer to collect or record that data.
(2) For the purposes of this section, “traffic data” means-
(a) information relating to communication by means of a computer system;
(b) the information generated by computer system that is part of the chain of communication; and
(c) information that shows the communication’s origin, destination, route, time, size, duration or the type of underlying service.

22. Mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha sheria ataharibu, atafuta, ataondoa, ataficha, atabadilisha au ataifanya data kompyuta kukosa maana kwa lengo la kuharibu ushahidi au kuchelewesha upelelezi atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini ya kiwango kisichopungua milioni tatu au kutumikia kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja au vyote.
(2) Mtu ambaye kwa makusudi atazuia utekeleza au atashindwa kutekeleza amri iliyotolewa na sheria hii, atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua mwaka mmoja au vyote.
Angalieni kipengele hiki pia:
Utoaji Data

32.-(1) Pale ambapo data inanitajika kuwekwa wazi kwa madhumuni ya uchunguzi wa kijinai au kuendeshwa kwa kesi mahakamani, Askari Polisi Mkuu wa kituo au afisa mtekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo anaweza kutoa amri kumtaka-
(a) mtu yeyote kuwasilisha data iliyoainishwa ambayo mtu huyo anaimiliki au iliyo chini ya uangalizi wake ambayo imehifadhaiwa kwenye mfumo wa kompyuta; au

(b) mtoa huduma yeyote, kuwasilisha taarifa kuhusiana na mteja zilizo kwenye umiliki au uangalizi wake.
(2) Iwapo kitu chochote kinachohusiana na upelelezi kinajumuisha data iliyohifadhiwa kwenye mfumo wa kompyuta au kwenye kifaa, amri itachukuliwa kumtaka mtu kutoa au kuruhusu upatikanaji wa data hiyo katika namna ambayo inasomeka na inayoweza kuondolewa.

No comments:

Post a Comment