Nikiwa katikati ya Tanzania.... Na hapa ni katikati mjini DODOMA na watanzania waliongea mengi kuhusu Maisha na maendeleo na pia ushiriki wao katikati kujenga nchi yetu.
Tutokevipi?
Nilipata bahati ya kula pamoja na famialia hii ya Singida na hapa ni mezani na chakula cha usiku kimeandaliwa na kuliwa... Ni watanzania hawa rafiki...
Tutokevipi?
Ni mwaka 2015 na watanzania wanakosha vyombo vya chakula cha mwanadamu katikati eneo hili... Ni kichanja cha kuosha na kuanika VYOMBO vya chakula.. Makao makuu ya TZ, DODOMA
Tutokevipi?
Bahati hutokea sio kila mtumishi wa ndani huteswa na mwajiri wake.. Hapana....
Huyu binti hajasoma hata darasa moja, ni mtumishi wa ndani.. Alikuja kwa mwajiri wake akiwa na miaka 4 na amekulia hapo na sasa ni boss wa mgahawa wa boss wake na hajawahi kukosea hesabu au kuyumbisha mgahawa wa boss wake... (mwajiri).
Tutokevipi?
HILO analochezea Dogo linaitwa ringi... Hutumika na familia duni kama mbinu ya kutuma mtoto dukani kwa haraka na pia kama mchezo wa watoto.
Tutokevipi?
Hili ni duka la matunda na mboga mboga. .. Hutumika kulea familia ya mke na watoto akitoka hapa... Baba katoka kazini na ni lazima apewe heshima.. .
Tutokevipi?
In 1987 Barack Obama at the age of 26 visited his father’s homeland for the first time. He met his brothers, sisters and grandmother and later he said, the visit was to transform his life. The images below come from that trip to connect with his African roots. What a transformation from an unknown young African man to the leader of the free world.
ONE DAY ' I WILL BECOME THE NEXT PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC .
Nikiwa na marafiki wanaoishi COMORO na hapo tulikua tukijadili njia sahihi za KUTOKA kwenye UMASIKINI .... !
Nikiwa kwenye vikao vya kawaida na wajumbe ... na bia moko moko bridiiiiiiiii '' eeh kwa mbali .
Nikiwa na familia ya kitanzania na hapo tulikua DODOMA katika ziara ya Tutokevipi? Na siku hii nilifurahisha familia hii.. Na mola awalinde wajane hawa... Ambao waume zao hawajafa.. Ila.....
Tulitembelea hospitali ya wagonjwa wa akili mirembe... Na tukajua kua sio waliowagonjwa wa akili tu bali hata wasio wagonjwa wa akili wanategemea hospitali hii.
Katika ziara yetu hii tuliwakumbuka wagonjwa wasio na ndugu.. . .
TUTOKEVIPI INSPIRATION .. SUMA ''
MAMA ZETU : KINA MAMA WAGONGA KOKOTO .. mmoja mwenye mwili kidogo , amesomesha mtoto mmoja mpaka chuo KIKUU , ujira wao kugonga mawe mpaka kujaza ndo moja ni ... shilingi 200 .
Nikiwa
na MHANDISI wa VIATU na tuliongea MENGI zaidi akiniambia anaishi vipi
kila siku kwa kazi hii ya UANDISI wa VIATU na kama inampa mahitaji yote
muhimu .
Rafiki
niliemchukua kunipeleka kwenye KAZI .. na hapa akinieleza mbinu za
kuendesha maisha yake na yapi kwake ni malengo ya BAADAE na kama anajua
atafikaje .
Chakula cha wengi ... Na HAPA nilikua nikienikieleza THAMANI YA ZIADA .. SEMINA YA TUTOKEVIPI? Bagamoyo .
Chakula cha mchana ... Madini ya CHUMA na viazi .
Rahisi na haraka .. jirani na Bahari
Tulifurahia
Zoezi la kutoa ELIMU ya THAMANI YA ZIADA na hapa tulipata ushiriki mzuri SANA .
Walikua watu wema .. TAHAMANI YA ZIADA iliwafaa sana .
Nikiwa na MTAALAM wa maswala ya Ardhi na mmiliki wa ENEO la KIJIWENI SINZA DAR es salaam ...
Pia alikua HAKIMU WA KANDA YA KASKAZINI wa mahakama ya ARDHI .
Nikiwa
na VIJANA Arusha tukiwa katika semina ya ADDED VALUE (THAMANI YA ZIADA )
na walituelewa sana hapa hakukua na mwenye swali na walikua kweli wapo
gizani .. hawa ni wataalam wa kutengeneza FRIJI .
Thamani
ya ZIADA ADDED VALUE kampeni ... Na hapa tulikutana na SEIGU ambae
pamoja na kua mlinzi anatumia sanaa kuishi mjini .. ni mtengenezaji wa
HALA za visu virefu maarufu kama SIME za kimaasai kwa kutumia MADUMU ya
mafuta ya chakula yaliyotumika .
Kijana
anaetumia DAWA za kulevya ... Ameachwa peke yake duniani familia yake
ya watu SABA wote wamekufa kwa SABABU tofauti na amebaki bila makazi
bila KAZI bila vision
Na bila msaada wowote , rafiki wake ni UNGA .
Nikiwa
na WATANZANIA wenzangu tukizungumza habari ya thamani ya ziada ndipo
tulipogundua kua , mmoja (kike) alikua ni muuza mchicha soko la mkoa wa
ARUSHA KILOMBERO na (Mwanaume) ni mpiga debe wa standi ila hapo alikua
likizo ya lazima isiyo na malipo ... Kwani alikua na MALERIA .
Vijana wanaotumia dawa za kulevya .... TULIZUNGUMZA NAO..
Foleni
ya kununua MIHOGO ... Hawa ni miongoni mwa watanzania wateja wengi sana
wa mihogo ... Na wanatengeneza ajira zisizo rasmi kwa wengi miji na
VIJIJINI ..
Na ni wanga ... Chakula
Vijana wa TANZANIA wakitafuta riziki na KODI ya serekali ...
Maeneo ya stendi ya mabasi ..
Kataa UMASIKINI .. Ratiba hii ilikua inafuatia baada ya kuuza VIAZI asubuhi kwa majirani na watoto wa AREA D DODOMA .
Na baada ya hapa ataenda sokoni na akirudi apike wale na aandae Viazi vitamu vya biashara KESHO .
Huyu
ni DEREVA wa boda boda aina ya baiskeli na hiki ni chombo chake cha
kubebea abiria ... Na anapata kipato cha kati ya sh. 6000 na 8000 kwa
siku kama itakua siku ilochangamka kibiashara ...
Huyu
ni baba wa familia na pato lake kwa siku mbaya ni sh. 3000 hadi 6000
kwa siku na mahitaji ya nyumbani kifamilia ni zaidi ya 8000 kwa siku
bila kua na akiba ya dharura yeyote ..
Arusha ...
Hawa
ni watafutaji vijana wa hali ya chini pato lao kwa siku ni chini ya
3000 kwa uhakika .. sahani moja ya wali au ugali ni bukumbli 2000 na
maji 600 mlo mmoja ...Dar es salaam
Huyu ni mfanya biashara wa zaidi ya miaka 20 ...
Hili ni duka lake ....
Hapa akionekana kwa nyuma ...
hapa akionekana kwa mbele ...
Huyu ni mfanaya biashara na Baba wa watoto tisa ... wote amewalea kwa nkazi hii .. na miongoni mwao wapo waliofika ngazi ya chuo kikuu na wengingine ni walimu .
hapa nilikutana nae akitokea KIMARA umbali wa zaidi ya kiliometa 11 na hapo ni SINZA na alikua akielekea MAGOMENI , MSASANI na badae anaelekea tena KIMARA kufuata malipo yake kwa MIGUU !..
Jina lake alikataa kabisa kunitajia .. ila aliniambia anatoka MOSHI .. na kwamba ana watoto wawili na hana mume anaishi mwenyewe na analea familia kwa kazi hii ...
Akijiandaa kupaki ... na kutoa huduma kwa duka linalotembea ...
MCHEZO WA USTADI WA UMILIKI GARI .. MICHEZO YA MBIO ZA MAGARI .. BAGAMOYO
NDEGE INAYOTUMIA MWANGA WA JUA KUPAA ... SIO MAFUTA WALA GESI ><><><><
Safari ya mwisho ya ndege ya kwanza inayotumia nishati ya miale ya jua kupaa angani, imetatizika kutokana na hali mbaya ya hewa.
Wataalamu wa utabiri wa hali ya anga, wamemuomba rubani wa ndege hiyo kusitisha kwa muda safari hiyo ili kuruhusu hali ya hewa kuwa shwari, ndipo aendelee na safari yake.
sorce BBC TAHADHARI TV ZA SUMSUNG ZINANASA SAUTI ><><><>>>
Samsung imewaonya wateja wake kuhusu kutojadili mambo yao ya kibinafsi mbele ya televisheni zao.
Onyo hilo ni kwa wale watazamaji ambao hudhibiti televisheni zao kwa kutumia sauti.Baadhi ya runinga hizo za kisasa husikiliza mambo ambayo wanasema na zinaweza kuwasilisha ujumbe kwa Samsung au mashirika yanayohusiana na Samsung kibiashara..
Onyo hilo limetolewa baada ya habari kuchapishwa katika gazeti la mtandao "Daily Beast" iliyochapisha sehemu ya sera za Samsung zinazosimamia umiliki wa kibinafsi wa televisheni zao.
Sera hiyo inaelezea kwamba televisheni hizo zitakuwa zinasikiliza watu katika chumba kimoja wakijaribu kutoa amri na maswali kutumia vibonyezi.
''Iwapo maneno ambayo umeyatamka ni ya kibinafsi au ya kisiri , basi ujue kuwa habari hiyo itakuwa kati ya habari zilizonaswa na kusambazwa kwa watu wengine.'' Samsung imeonya
Kutokana na kukabiliana kuhusu taarifa ya sera yake ,Samsung imetoa taarifa kufafanua jinsi sauti hizo zinavyofanya kazi.
Inasisitiza utambuaji wa sauti unajulikana tu baada ya mmiliki kuchagua kutumia sauti badala ya kubonyeza kifaa cha kiungia mbali (remote control)
Samsung imesema kama mteja atakubali kutumia kifaa cha kugundua sauti, sauti hiyo itatambuliwa na mtu wa upande wa tatu baada ya amri ya kuitafuta sauti hiyo.
Upande watatu ambao unatafsiri sauti kutoka kwa wamiliki hufasiriwa na kampuni inayoitwa Nuance, ambayo imehitimu kutambua sauti.
Samsung si kampuni ya kwanza kujipata mashakani kwa kutumia vinasa sauti kwenye mashine na bidhaa zake.
Mwishoni mwa mwaka wa 2013,mshauri wa maswala ya kiteknolijia kutoka Uingereza aligundua kuwa televisheni yake ya LG ilikuwa inakusanya habari kuhusu tabia yake ya utazamaji wa televisheni.
UTAFITI WAONYESHA VIRUSI VYA UKIMWI KUKOSA NGUVU ..><><><><><><
Utafiti mkubwa wa kisayansi
umeonyesha kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi vya HIV,
vinapungua makali yake na kushuka kwa uwezo wake wa maambukizi kwa jinsi
vinavyobadilika.
Kikosi hicho cha madaktari kimegundua kuwa virusi vya HIV vilikuwa vikiingia katika hatua ya kuharibu mabadiliko yake ili kuishi na kwa kufanya hivyo, virusi hivyo kwa sasa vinabadilika taratibu zaidi na inavichukua muda mrefu zaidi kusababisha ugonjwa wa UKIMWI kwa watu wenye kuishi na virusi hivyo.
Wanasayansi hao wamesema kupungua kwa makali ya virusi vya HIV kutaweza kusaidia jitihada za kutokomeza virusi hivyo, japokuwa wameonya kuwa virusi hivyo dhaifu bado ni hatari kwa afya ya binadamu
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, Desemba Mosi ya kila mwaka, takwimu zinaonyesha juhudi zilizofanyika katika kupambana na ugonjwa huo.
Maambukizi ya virusi vya Ukimwi yameshuka kwa asilimia 38 tangu mwaka 2001 na idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi vimepungua kutoka zaidi ya milioni 2.3 mwaka 2005 hadi milioni 1.5 mwaka 2013.
Haya yakiwa maendeleo mazuri, bado idadi kubwa ya watu wapatao milioni 35 wanaishi na virusi vya Ukimwi. Kila siku zaidi ya watu 5,700 wanaambukizwa virusi vya Ukimwi, sawa na watu karibu 240 kila saa.
Ifikapo mwaka 2015, watoto milioni 25 watapoteza mzazi mmoja au wote wawili kutokana na ugonjwa wa UKIMWI.
Ugonjwa huu ni janga kubwa la kijamii duniani.
UKIWMI si tu unawanyang'anya mamilioni ya watoto maskini kabisa, upendo na ulinzi kutoka kwa wazazi wao, bali pia watoto wengiwanabakia kuhangaika peke yao, wengi wakiwa na jukumu la kuwalea wadogo zao, katika hali ya umaskini mkubwa, kubaguliwa na unyanyapaa unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya HIV.
Watoto wengi wanatengwa na mara nyingi ndugu wa familia zao hawawezi kuwatunza.
Muasisi wa kampuni ya Microsoft,
Bill Gates, anasema anaamini kuwa idadi ya watu wanaougua UKIMWI inaweza
kupungua kwa zaidi ya 95% katika miaka 15 ijayo, iwapo chanjo na dawa
za kutibu ugonjwa zitafanikiwa kutengenezwa.
Mfuko wa Bill na Melinda Gates umetumia mamilioni ya dola kugharimia utafiti kuhusu UKIMWI.
SOKWE WAPISHI ....><><><><
Wanasayansi kutoka Marekani wana
imani kuwa sokwe wana uwezo na akili ya kupika chakula. Wanasayansi hao
wamefanya baadhi ya majaribio ambayo yameonyesha kuwa sokwe wanaweza
kupika mboga za majani na wana uwezo wa kuhimili kusubiri chakula cha
moto.
Hivyo wanachokihitaji sokwe ni ujuzi wa upishi kwani imedhihirika kuwa wana uwezo wa kuhimili moto.
No comments:
Post a Comment