Monday, 13 June 2016
Saturday, 4 July 2015
LOADED .... TUTOKE VIPI ?
Mambo vipi Rafiki wa TUTOKEVIPI? ...
LEO... Tuangalie maisha ya kweli mtaani.. Majumbani kwa watu, wanavyoishi na namna hali hii inavyoweza kuathiri maisha ya watu wote na AMANI ya nchi.
Nikiwa DODOMA nilikutana na kijana ambae kazi yake ni wizi wa mfkoni, na pia ameshiriki matukio kadhaa ya kihalifu yenye madhara makubwa sana na yasiyosimulika...
Lakini sio kwa kupenda kua mwizi.. No! Ila kwa kupambana na maisha..
Aliwahi kuchukuliwa kwa ahadi ya kua muuza duka... Kule akawa mchunga mbuzi.. Akakata kidole akikatia mbuzi majani.. Mama mwajiri akamwambia weka spirit itapona... Kwa uchungu akauza gunia la mahindi akaamsha..
Kuja tena dom hana ramani.. Pa kulala hana pa kula hana.. Njaa ataishije.. Akaanza kabali mtaani AMANI imesepa.. Tatizo.
Haya umemaliza chuo unakazi.. Ila mshahara Lakini tatu na 80, ndio kwanza unaanza kick ya maisha alafu kuna vitu kama kula bata, na kuandaa pa kuishi mavazi, nauli, na hapo hapo maza anakwambia mwanangu wadogo zako hawana hiki hiki.. Na maza hana kitu.. Hapo bado demu wako hajaanza kelele ka' cm ya kichina.. Alafu ww mshahara laki tatu tu.
Na ofisini kuna madili...
Tafuta tofauti kati yako na huyu kijana .
KATAA UMASIKINI
Hon. E. LOWASSA
Hon. E. LOWASSA
Friday, 26 June 2015
ENYEMA na KOCHA WAWEKWA KITI MOTO ....!
Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) limewaweka kitimoto kipa wao mkongwe, Vincent Enyeama na kocha Stephen Keshi kwa madai ya utovu wa nidhamu na kukiuka kanuni za maadili walizosaini.
Enyeama, 32, anayeongoza kwa kuchezea zaidi timu ya taifa – Super Eagles, anashitakiwa kwa kusema hadharani kwamba hawakutakiwa kucheza jijini Kaduna dhidi ya Chad, akieleza kwamba usalama haungekuwapo.
Hiyo ilikuwa wakati wa mechi ya kwanza ya kutafuta kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017. Keshi anatakiwa kujibu mashitaka ya kuomba kazi ya kuifundisha Timu ya Taifa ya Ivory Coast, muda mfupi tu baada ya kupewa kazi ya kudumu na NFF.
Enyeama anasema kwamba alidhani suala lake limemalizika kwa sababu alitakiwa aombe radhi na kufanya hivyo mara moja, lakini sasa NFF inahoji kwa nini hakufika kwenye kikao cha kusikiliza kesi yake wiki hii.
Kipa huyo anasema kwamba wala hajapata barua inayomwita kwenye kikao hicho. Keshi kwa upande wake anadai kwamba hajapata kuomba kazi Ivory Coast, bali wakala ambaye hata hivyo hakumtaja jina, ndiye alipeleka maombi hayo bila kumuarifu.
Ivory Coast wanatafuta kocha kwa ajili ya timu yao ya taifa – Tembo – na baada ya makocha au mawakala kutuma maombi, shirikisho la soka la huko lilibandika hadharani majina ya makocha 59 walioomba, wakiwamo Wafaransa na Waitaliano wengi, Mwingereza mmoja na Keshi.
Ivory Coast wanatafuta mrithi wa Herve Renard aliyewapa ubingwa wa Afrika na kisha kuondoka kwa ajili ya kufanya kazi nchini Ufaransa.
Ofisa wa ngazi za juu wa NFF, Chris Green amenukuliwa na vyombo vya habari vya Nigeria akisema kwamba watatuma ujumbe Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya kupata ukweli juu ya uombaji kazi wa Keshi kabla ya shauri lake kusikilizwa.
Kamati ya Utendaji ya NFF itatoa uamuzi baadaye juu ya mchezaji na kocha huyo, lakini bado haijasema ni lini itafanya hivyo. Mechi nyingine ya kufuzu kwa AFCON baina ya Nigeria na Misri imepangwa pia kufanyika jijini Kaduna.
Nigeria imekuwa ikiandamwa na mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa genge la Boko Haram katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, na ni kwa sababu hiyo Enyeama alitaka mechi ifanyike eneo lenye usalama zaidi.
FISI ALA WATOTO .. BAHI ...!
Bwana FISI akiwa katika mawindo yake ya kawaida ...
Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.
Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala. “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta (mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,”alisema Mwaja.
Alisema usiku wa kuamkia jana, fisi huyo alirudi tena katika kijiji hicho na kumnyang’anya mama mmoja mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili.
Mwaja alisema fisi huyo alimla mtoto huyo na kumbakisha kichwa na utumbo tu, hali iliyozua taharuki katika kijiji hicho.
Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo wananchi waliamua kufanya msako na kumkamata fisi huyo na kumuua.
Baba mzazi wa mtoto aliyeuawa usiku wa kuamkia jana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mchamingi, alisema hawana imani kama fisi huyo kama ni wa kawaida kwani katika tukio la kwanza kabla ya kuuawa, alikimbilia katika kijiji jirani cha Bahi Makulu na kupotelea kwenye nyumba za watu.
HAT-TRICK YA GUERRERO ‘PREDETOR’ IMEIPELEKA PERU NUSU FAINALI YA COPA AMERICA KIULAIIINI .. toka SHAFII DAUDA
Goli tatu ‘hat-trick’ ya Paolo Guerrero ‘Predetor’ dhidi ya Bolivia inaipeleka Peru kiulaini kwenye nusu fainali ya michuano ya Copa America 2015 inayozidi kushika kasi huko nchini Chille baada ya Peru kuibuka na ushindi murua wa goli 3-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa usiku ‘mwingi’ wa Alhamisi kuamkia leo (Ijumaa).
Zilimchukua dakika 20 tu Guerrero ambae ni straika wa klabu ya Corinthians kupachika bao la kwanza na kuanza kuitafuta hat-trick yake kwenye michuano hiyo akiunganisha krosi safi kutoka kwa Romel Quinonez. Dakika tatu baadae mkali huyo alizama tena wavuni kupiga goli la pili kabla hajashindilia msumari wa mwiso dakika 16 kabla ya mchezo kumalizika. Mshambuliaji wa zamani wa Wigan Athletic Marcelo Moreno aliipatia Bolivia goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati na mchezo huo kumalizika kwa Peru kutinga fainali kwa ushindi wa goli 3-1.
Ushindi huo unaifanya Peru ikumbane na wenyeji Chile kwenye mchezo wa nusu fainali ya mashindano hayo ya Copa America kwenye dimba la Santiago siku ya Jumatatu Juni 29 mwaka huu kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza hatua ya fainali.
Imebaki michezo miwili ya robo fainali ili kukamilisha timu nne za kukipiga kwenye michezo miwili ya nusu fainali, Argentina itakipiga dhidi ya Colombia Jumamosi Juni 27 kwenye mchezo wa robo fainali wakati siku hiyo pia Brazil itakuwa ikimenyana na Paraguay kwenye mchezo mwingine wa robo fainali.
Thursday, 25 June 2015
MAKAMU WAKE WA RAIS KALAZA .. SPIKA WA BUNGE , .. KALAZA ! BADO NKURUNZINZA ANAKWAMBIA .. UCHAGUZI UPO PALE PALE .. dyu !
Gervais Rufyikiri aliyekuwa makamu wa rais wa Burundi amekimbilia Ubelgiji.
Serikali ya Burundi imesema haitashiriki katika mazungumzo yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakilenga kupunguza hali ya uhasama uliopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wenye utata.
Maandamano yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadha kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania nafasi ya urais kwa mara ya tatu.
Wote wawili wamekuwa wakosoaji wa rais. Uchaguzi umepangwa kufanyika mwezi uajao. Uchaguzi wa wabunge unafanyika Jumatatu.
SHUTUMA KWA POLISI WA SA .... WALIUA RAIA WAKUTOSHA !
polisi afrika ya KUSINI .
Tume ya uchunguzi nchini Afrika kusini imetaka ufanyike uchunguzi dhidi ya Polisi kuhusu mauaji ya wafanyakazi 34 wa mgodi yaliyofanyika mwaka 2012.
Wakati wote Polisi wamekuwa wakidai kuwa walikuwa wakijihami wakati wa mgomo wa wafanyakazi waliokuwa wakidai kuongezwa kwa mishahara.
Mauaji ya Marikana yanaelezwa kuwa mabaya kutokea nchini Afrika kusini tangu baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi miaka 20 iliyopita.
Wafanyakazi wa mgodi waligoma kwa siku kadhaa,na watu 10 tayari walipoteza maisha wakiwemo watu ambao hawakuwa kwenye mgomo, walinzi wa mgodi na Polisi, kabla ya tukio la tarehe 16 Agosti.
Subscribe to:
Posts (Atom)