Shirikisho la soka la Ghana limetoa maelezo kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amepumzishwa hospitali katika mji wa Mongomo tangu Jumamosi jioni na kuruhusiwa Jumapili asubuhi ,na inaelezwa kuwa maradhi hayo yametibiwa katika hatua za awali na mchezaji huyo anaendelea vyema.
Na upande wa Senegal,Alain Giresse anapaswa kufanya maamuzi juu ya afya ya Sadio Mane, ambaye alikuwa nje ya dimba kutokana na kigimbi chake kuumia.Sadio ni mchezaji wa timu ya Southampton na alijumuishwa katika kikosi cha Senegal pamoja na kwamba timu yake iligoma kwa maelezo kwamba hatakuwa sawa kiafya.
Lakini Giresse ameendelea kushikilia msimamo wake kwa kusema kama hataweza kucheza katika mechi za awali,itakuwa maraya ya pili kama si ya tatu tutaangalia maendeleo ya hali yake.
Kwa upande wake Sadio yeye,anaeleza kuwa alikuwa na ndoto ya kuichezea timu yake ya taifa katika kombe hilo la mataifa ya Afrika na kipaumbele ni timu ya Taifa na West Ham baadaye.kwa heshima alonayo kwa klabu yake,wanaheshimu uamuzi wake endapo kama asingekuwa na maumivu hayo, ni fursa pekee ambayo mtu yeyote asingependa kuikosa.
Lakini walau analo chaguo, anaweza kumwita mchezaji wa timu ya Marseille ,mchezaji wa mbele Andre Ayew na pia mchezaji wa timua ya Everton Christian Atsu ama hata Mubarak Wakaso wa timu ya Celtic.
No comments:
Post a Comment