Thursday, 22 January 2015

SEREKALI YAKANA KUUWA WAANDAMANAJI KONGO ..

Serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekanusha madai ya kuwauwa waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga mapendekezo ya kubadilisha sheria za uchaguzi mkuu.

Makundi ya kutetea haki za binadamu, yanasema kuwa zaidi ya watu arubaini wameuawa katika siku tatu za ghasia.


Waziri wa mawasiliano Lambert Mende, aliambia BBC kwamba polisi hawakutumia silaha zozote dhidi ya waandamanaji hao.


Alisema waandamanaji ambao aoliwataja kama waporaji, waliuawa na walinzi waliokuwa wanalinda majengo ya biashara yaliyoporwa.


Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kwamba zaidi ya watu 40 wameuawa katika siku tatu za vurugu mjini Kinshasa.


Mabadiliko yaliyopendekezwa huenda yakachelewesha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao, wakati Kabila anatarajiwa kung'atuka baada ya kuitawala nchini huo kwa miaka 14.

No comments:

Post a Comment