Tiger wood amepoteza jino lake la mbele juu baada ya kugongwa na kamera wakati akimtazama mpenzi wake Lindsey Vonn akinyakua kikombe cha ushindi
Nguli huyo wa zamani wa mchezo wa gofu, aliamua kwenda katika michuano ya kuteleza kwenye barafu ili kumshangaza Vonn mpenziwe ambaye alikuwa hamtarajii kumwona akichuana Cortina d’Ampezzo huko Italia.
Baada ya kwisha kwa michuano hiyo ya kuteleza barafuni, watu wakajisogeza karibu na mimbari ya kutolea tuzo,waandishi ili kutaka kupata picha nzuri wakawa wakisukumana ndipo mwandishi mmoja aliposukumwa namwenziwe kiasi cha kuteleza kutoka mimbarini na kamera kumtoka na kumgonga Tiger Woods mdomoni,na wakala ya nguli huyo wa zamani wa mchezo wa golfu alieleza hali hiyo kuwa aligongwa kwa bahati mbaya
No comments:
Post a Comment