Friday, 23 January 2015

UNAWAKUMBUKA ROMEO NA JULIETH WA KENYA (MHINDI NA MSWAHILI) ..>>

 

Je unakumbuka kisa cha wapenzi wawili waliozua gumzo nchini Kenya?
Msichana mhindi Sarika Patel kutoka familia tajiri na Timothy Khamala mbukusu kutoka familia maskini kutoka Magharibi mwa Kenya kuoana? wakati yao mapenzi yao yalijulikana kama Bukusu Darling, sifa kwa wanakoishi wawili hao.

Taarifa sasa ni kwamba mapenzi yao yamefika kikomo. Familia ya msichana Sarika ililaani sana mapenzi hayo kwani Timothy alikuwa anafanya kazi kwao kama mfanyakazi wa nyumbani.
Na Sarika alipoamua kwenda kuishi na Timothy kama mume na mke familia yake ilimfukuza na kisha kumfuta kazi Timothy.

Wawili hao walioana kinyume na matakwa ya familia ya Sarika ambayo kwao ilikuwa ni kama aibu kubwa sana kwa mtoto wao kutoka familia tajiri kuolea na kijana asiyekuwa na mbele wala nyuma.
Wakati taarifa ya wawili hao ilipogonga vichwa vya habari nchini Kenya, Sarika na mume wake walipata kazi katika kiwanda cha kutengeza Sukari kutoka kwa wahisani.

Lakini sasa kuna madai kwamba ndoa yao imevunjika baada ya Sarika kulalamika kwamba Timothy amekuwa akimdhulumu na kumtusi kila mara hali iliyosababisha wawili hao kutalakiana.
Mtandao wa Standard Digital umemnukuu Sarika akisema: "nilipokuwa mgonjwa , hakuwa hata na muda wa kunipeleka hospitalini badala yake wazazi wake ndio walionipeleka kutafuta matibabu. Mbali na hayo amekuwa akinichapa, '' alisema Sarika huku akibubujikwa na machozi.

Kwa sasa inaarifiwa anajuta sana kwa nini alikaidi amri ya wazazi wake.

''Ninajuta sana kwa nini sikuwasikiliza wazazi wangu na kuolewa kinyume na mapenzi yao. Ninaomba radhi, natumai watanikubali kurejea nyumbani. ''
Sarika ambaye ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano, ameamua kurejea nyumbani na kusema kamwe hatawahi kuwa na uhusiano wa kimepenzi tena. Lakini wazazi wake wamempa masharti, mwanzo aishi na rafiki yake huku akifanya uamuzi wa mwisho kuhusu anakotaka kuishi.

Anasema anahofia kwamba jamii ya wahindi haitamkubali tena kwani hakuwasikiliza wakati walipomshauri kutoolewa na mwanamume mwafrika.

No comments:

Post a Comment