Mustakabali wa kipa David de Gea
kusalia Manchester United upo shakani baada ya wakala wake Jorge Mendes
kushindwa kuwakatalia Real Madrid mpango wa kumsajili.
Manchester United inajianda kutoa
ofa kwa timu ya Villarreal ili kumpata kumpata beki Gabriel Paulista, raia wa
Brazil ambae yuko kwenye mazungumzo na Arsenal.
Klabu ya Chelsea iko katika
mipango ya kumsajili kiungo wa Shakhtar Donetsk Douglas Costa.
Bosi wa West Brom Tony Pulis
imethibitisha kuhitaji kuwasajili winga wa Wigan Callum McManaman na kiungo
Darren Fletcher toka Man United katika dirisha hili la usajili.
Timu ya QPR imetoa ofa ya kumsajili
mshambuliji wa zamani Ac Milan Alexandre Pato,anayechezea timu ya Sao paul kwa
mkopo.
Meneja wa Swansea City Garry
Monk anavutiwa na mpango wa kumsajilibeki wa kushoto wa Norwich Martin Olsson,
mwenye miaka 26,pamoja na kiungo Alexandru Maxim toka Stuttgart
Kipa wa Manchester United David da
Gea
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers
anatarajia winga wake Raheem Sterling, atasaini mkataba wa muda mrefu kusalia
klabu hapo siku chache zijazo.
Manchester City wameulizia uwezekano
wa kumpata mshambuliaji Jay Rodriguez wa timu ya Southampton.
Hull City wanamfuatilia winga wa
Tottenham timu Taifa ya England Aaron Lennon,ambae anataka kuondoka White Hart
Lane kwa kukosa namba kikosi cha kwanza.
Kiungo wa zamani wa Chelsea
Kevin de Bruyne,amekata kurejea katika ligi ya England kwa kusema havutiwi
kurudi katika ligi pamoja na kwepo taarifa za kuwaniwa na Arsenal na Manchester
United.
Klabu ya Roma inajaribu
kiwashawishi Chelsea kukubali pauni 380,000 ili kumchukua winga Mohamed Salah
kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.
No comments:
Post a Comment