Sunday, 18 January 2015

AJALI MBAYA YA MABASI YATOKEA ZIMBABWE LEO ... 25 WAFARIKI

Ajali mbaya ya mabasi mawili ya abiria imetokea nje kidogo na mji mkuu wa ZIMBABWE , Harare .
Polisi wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba watu 25 walifariki pale pale baada ya mabasi mawili kuvaana uso kwa uso (head - on collusion ) .
Abiria wengine 45 waliumia vibaya na kuwahishwa hospitalini kwa matibabu .

Ni kilomita 35 kutoka Harare , bara bara ya Nyamanpanda natari sana kwa mwendo kasi , inaonekana madereva walizembea na ndio sababu ya ajali hii ., hatujajua kama waliopoteza maisha au kujeruhiwa wamo madereva ila uchunguzi wa polisi umeonyesha kuwapo na uzembe wa madereva .

Hakukua na mvua na mwanga ulikuapo wa kutosha , hakukua na giza alisema msemaji wa polisi CHARITY CHARAMBA .

Charamba pia aliongeza kua watu 24 walifariki papo hapo na mwingine mmoja alifariki akipelekwa Hospitali.

Pia aliyataja mabasi hayo kua ni Zimbabwe United Passenger Company (ZUPCO) na Unifreight Africa Limited,  Harare-Nyamanpanda highway.
Bara bara hii imetajwa kua hatari kwa kua na ajali nyingi toka mwaka 2009

No comments:

Post a Comment