Friday, 23 January 2015
BAADA YA MACHOZI YA MABOMU .. WANA KIBINDANKO'I SASA SHANGWE ..>
Baraza hilo la Senate lilipiga kura kurekebisha mswada huo tatanishi uliopendekeza sheria za uchaguzi kufanyiwa mabadiliko. Limefuta kipengee kinachohitaji kufanyika kwa sensa kote nchini kabla ya uchaguzi kufanyika mwaka ujao.
Mswada huo ndio uliozua vurugu na ghasia katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kwa wiki moja.
Mabadiliko hayo sasa yanafuta kipengee ambacho kingechelewesha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.
Wapinzani wa Rais Joseph Kabaila wanasema hii ni njama ya Rais kufanya mageuzi ya kikatiba hali ambayo itampa fursa Kabila kusaialia madarakani kwa muhula mwingine.
Kura ya mwisho kuhusu mswada huo itafanyika wiki ijayo katika bunge la waakilishi na baraza hilo la Senate.
Huduma ya internet sasa imerejeshwa nchini humo, katika juhudi za serikali kusitisha vurugu ingawa mitandao ya kijamii bado imevurugwa ili kutatiza mawasiliano.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu 40 waliuawa katika vurugu hizo ingawa serikali imepinga madai hayo.
Mkuu wa baraza hilo alitaja uamuzi huo kama wa kihistoria na kusema kuwa masenta walisikiliza kilio cha wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment