Matokeo ya kura za urais nchini Zambia sasa yameanza kukamilika katika ukumbi wa kimataifa wa Mulungushi makao makuu ya kuhesabia kura .
Matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi ya Zambia Usiku wa kuamkia leo yanaonyesha kuwa Edgar Lungu mgombea wa chama tawala cha
Patriotic Front mpaka sasa bado anaongoza akiwa na kura 670397 huku mpinzani wake HakaindeHachilema wa chama cha United Party for National Development akiwa karibu sana nae kwa kura 641343.
Hivo Edgar Lungu anaongoza kwa 48.8 % na hali Hakainde Hachilema akiwa na 46,9 % na Bi Nanakwi mwanamke pekee kwenye kinyanganyiro hicho yuko nafasi ya 3 akiwa na kura 11 260 (0. 268 % )
Kwa jumla kura million 1 371 778 ndizo zimeisabiwa kutoka majimbo 111 ikiwa sasa imebakia majimbo 39 tu
No comments:
Post a Comment