Tuesday, 20 January 2015

MAMBO MUHIMU KUJUA KAMA U MTAFUTAJI .... >>

Shirika la kimataifa la kutoa misaada la Oxfam limesema leo kuwa asilimia moja ya watu walio matajiri zaidi duniani watamiliki nusu ya mali yote duniani ifikapo mwaka ujao.

 Oxfam imetoa ripoti hiyo kabla ya mkutano wa jukwaa la kiuchumi duniani kuanza Jumatano mjini Davos, Uswisi.

Shirika hilo limesema matajiri zaidi duniani walishuhudia ukuaji wa mali zao mwaka jana kwa asilimia 48 kutoka asilimia 44 ilivyokuwa mwaka 2009.

Kuzidi kupanuka kwa pengo kati ya maskini na matajiri duniani kunatatiza juhudi za kupambana na kutokuwepo usawa.

Oxfam imesema wakati matajiri wakizidi kutajirika, watu tisa kati ya kumi duniani hawana chakula cha kutosha na zaidi ya watu bilioni moja wanaishi chini ya pato la dola moja kwa siku

No comments:

Post a Comment