Algeria, Ghana robo fainali AFCON 2015
January 28, 2015
Chelsea wawapiga Liverpool
Chelsea wamekata ngebe za Liverpool
baada ya kuwafunga 1-0 kwenye mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Kombe
la Ligi.
Chelsea ambao hawajafungwa katika mechi sita dhidi ya Liverpool, na ambao walitoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza Anfield, walipata bao dakika ya 94 kupitia kwa Branislav Ivanovic.
Liverpool hawajapata kufika fainali yoyote ya michuano ya hapa nyumbani tangu 2012 na kwa ushindi wao, Chelsea watakabiliana kwenye fainali na ama Tottenham Hotspur au Sheffield United wanaocheza leo.

Ivanovic alikwenda juu na kufunga
bao zuri la kichwa, akiwapeleka Chelsea Wembley kwenye michuano hii ya Capital
One Cup ambayo ni midogo kwa Ligi Kuu na ile ya Kombe la FA.
Hadi dakika 90 zinamalizika timu zilikuwa suluhu, hivyo kupelekwa kwenye dakika 30 za nyongeza, na laiti zineshindwa kufungana au kama zingetoka sare, basi changamoto ya penati ingeanza.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho hakuona bao lao lilivyoingia, kwani alikuwa akizozana na mwamuzi wa akiba, Phil Dowd.

Walau matokeo haya yatakuwa faraja
kwa Chelsea walioaibishwa kwa kufungwa na timu ndogo ya Bradford City 4-2 na
kutupwa nje ya michuano ya Kombe la FA, ambapo walikuwa na ndoto ya kutwaa
makombe manne, yaani ubingwa wa England, Kombe la FA, Kombe la Ligi na ubingwa
wa Ulaya msimu huu.
Liverpool waliondoka Stamford Bridge wakiwa wanajutia kukosa nafasi kadhaa, hasa aliyopata Jordan Henderson, kwa mpira wa kichwa akiwa na lango wazi mbele yake.
Liverpool waliondoka Stamford Bridge wakiwa wanajutia kukosa nafasi kadhaa, hasa aliyopata Jordan Henderson, kwa mpira wa kichwa akiwa na lango wazi mbele yake.
Lakini Chelsea wanaweza kuadhibiwa
vikali iwapo mamlaka husika zitaridhia, kwani mshambuliaji wao Diego Costa
alifanya makosa mawili ya wazi na makusudi dhidi ya Emre Can na Martin Skrtel
kwa kuwakanyga, na yote hayakuonwa na mwamuzi Michael Oliver.
Algeria, Ghana robo fainali AFCON
2015
Algeria na Ghana wamevuka kihunzi
cha kundi lao na kuingia hatua ya mtoano kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika (AFCON).
Andre Ayew alifunga bao la ushindi dhidi ya Afrika Kusini dakika za mwisho akipokea majalo murua ya Baba Rahman kutoka wingi ya kushoto.
Andre Ayew alifunga bao la ushindi dhidi ya Afrika Kusini dakika za mwisho akipokea majalo murua ya Baba Rahman kutoka wingi ya kushoto.
Kocha Avram Grant alifarijika sana
na matokeo hayo, akiona kwamba ni nyota njema, licha ya Afrika Kusini
kutangulia kupata bao kupitia kwa Mandla Masango, bao linaloweza kuwa bora
katika mashindano haya, akifunga kutoka umbali wa yadi 25.
Hata hivyo Ghana walitia shinikizo
kwa wapinzani wao na akitokea benchi, John Boye aliwafungia bao la kusawazisha,
dakika 17 tu kabla ya mpira kumalizika, wengi wakijua kwmaba Ghana walikuwa
wakielekea nyumbani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ghana
kuwafunga Afrika Kusini kwenye mechi za AFCON lakini waliianza mechi
wakionekana walitaka kushinda.
Hata hivyo, bao la Ayew liliwahakikishia kuvuka, tena wakiwa wa kwanza kwenye kundi hilo, wakivuka pamoja na Algeria ambao waliwatungua Senegal 2-0.
Hata hivyo, bao la Ayew liliwahakikishia kuvuka, tena wakiwa wa kwanza kwenye kundi hilo, wakivuka pamoja na Algeria ambao waliwatungua Senegal 2-0.
Algeria walipata mabao yao kupitia
kwa mchezaji wa Leicester, Riyad Mahrez na msumari wa mwisho kwenye jeneza la
Senegal ukatiliwa na mchezaji wa Tottenham Hotspur, Nabil Bentaleb, akipiga
mkwaju wake kutoka yadi 18.
Algeria walionesha soka safi muda
wote wa mchezo lakini walipata pigo kwa nyota wao, Yacine Brahimi kuumia dakika
ya 72 na kulazimika kutolewa nje.
No comments:
Post a Comment