Waziri mkuu wa JAPAN SHINZO ABE amelazimika kukimbia nyumbani kukabili kiweledi utakaji nyara na tishio la kuuwawa kwa wanchi wawili wa Japan na waasi wa IS .
Waasi hao waliokaririwa wakisema “Ni muda sasa serekali yenu ichukue hatua juu ya maisha yenu “ .
Watekaji hao wamedai kiasi cha $200 millioni ili kuwaachia huru mateka wawili wa kijapani .
Iwapo mateka hao watauwawa waasi wa IS , syria na IRAQ wanaweza kuvaa joto kali zaidi la mapambano .
Waziri ABE amesema , Japan haina mpango wa kusikilizana na magaidi wowote duniani na kwamba waasi hao wawaachie mateka hao wawili wa kijapan bila masharti yeyote na bila kuwadhuru .
Aliyasema hayo akiwa ISRAEL .
Picha zilizopatikana zinamuonyesha mtekaji nyara akiwa katika mavazi meusi yaliyofunika kabisa uso wake na akiwa na kisu cheusi mkononi mwake , upande wa kulia akiwa raia wa japan aliyevikwa nvazi la rangi ya chungwa na mwingine upande wa kushoto .
No comments:
Post a Comment