Tuesday, 20 January 2015

CONGO HALI TETE ... NIA YA KABILA KUWANIA URAIS TENA !

Maafisa wa usalama katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamewafyatulia risasi na gesi ya kutoa machozi waandamanaji waliokuwa wakiandamana katika mji mkuu Kinshasa, hii leo kupinga kufanyiwa marekebisho sheria za uchaguzi kuruhusu kufanyika kwa zoezi la kuwahesabu watu nchini humo, zoezi ambalo litachelewesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka ujao. Watu kadhaa wanaripotiwa kujeruhiwa kutokana na ufyatulianaji huo. Maandamano kama hayo pia yamefanyika katika mji wa mashariki mwa Kongo wa Goma. Viongozi wa upinzani waliitisha maandamano hayo kupinga zoezi hilo la sensa kufanyika wakati huu kwani huenda likasababisha kucheleweshwa kwa uchaguzi na hivyo Rais Joseph Kabila atasalia madarakani kwa muda mrefu.Viongozi wa upinzani hawakuweza kujumuika na waandamanaji kwani ofisi zao zimezingirwa na askari.

No comments:

Post a Comment