Waziri Mkuu wa Uingereza, David
Cameron, amepinga matamshi ya Papa ya juma lilopita aliposema kuwa siyo
sawa kufanya mzaha juu ya imani ya watu wengine.
Bwana Cameron hata hivyo alisema katika nchi huru kuna haki ya kukera kuhusu dini ya mtu mwengine.
Aliliambia shirika la habari la CBS la Marekani, kwamba vyombo vya habari vinafaa kuweza kuchapisha vitu ambavyo vinawakera baadhi ya watu - ikiwa siyo kinyume na sheria.
No comments:
Post a Comment