Monday, 26 January 2015

THELUJI YATISHA MIJI MIKUBWA HUKO MAREKANI ...>>


mashirika ya ndege yamesitisha kwa muda huduma zao kwa jamii
27.01.2015 06:41
Dhoruba kubwa ya theluji inatarajiwa kuathiri  sehemu kubwa ya kaskazini- mashariki mwa Marekani katika siku mbili zijazo ikianza kupiga maeneo makubwa ya mijini kutoka Washington DC  hadi Boston jumatatu.
Kiwango kikubwa cha dhoruba kilikwepa mji mkuu wa Marekani  lakini ilipiga  upande wa  kaskazini kwenye majimbo ya New Jersey, New York, Connecticut, Rhode Island na Massachusetts ambapo walitangaziwa hali ya dharura kutokana na theluji.
Mamilioni ya watu waliombwa kukaa nyumbani wakati usafiri wa reli wa Amtrack ulipunguza huduma za treni katika maeneo yenye shughuli  nyingi katika ukanda wa kaskazini mashariki  yaani Northeast Corridor na mashirika ya ndege yalifuta  mamia ya safari za  ndege katika kujiandaa na hali ya dhoruba jumatatu usiku hadi jumatano

No comments:

Post a Comment