Jeshi la Cameroon limeweza kuwaachia huru watu 24 waliokuwa wametekwa
nyara na waasi wa kundi la Boko Haram.
Waasi wa Boko Haram hapo jana
walivivamia vijiji kadhaa kaskazini mwa Cameroon na kuwateka nyara kiasi
ya watu themanini, wengi wao wanawake na watoto katika mojawapo ya
mashambulizi makubwa kufanywa na Boko Haram katika nchi hiyo jirani na
Nigeria.
Msemaji wa jeshi la Cameroon Kanali Didier Badjeck amesema
wanajeshi walifanikiwa kuachiwa huru kwa mateka 24 wakati walipowafuata
waasi hao waliokuwa wakitoroka nao kuelekea Nigeria.
Boko Haram imewaua
maelfu ya watu kaskazini mwa Nigeria tangu ilipoanzisha uasi na waasi
hao wametanua uasi wao hadi nchi jirani za Cameroon na Niger.
Chad
imeyatuma majeshi yake katika nchi hizo kama sehemu ya juhudi za pamoja
kupambana na Boko Haram.
No comments:
Post a Comment