- Dakika 26 zilizopita
Sio kawaida kwa ziara alizopangiwa
Rais wa Korea Kaskazini kutangazwa hadharanbi kabla ya safari.
Serikali ya Urusi inasema kwamba
Rais wa Korea Kaskazini amekubali mwaliko wa Rais wa nchi hiyo kuzuru Urusi.
Taarifa hii ni ka mujibu wa shirika
la habari la Yonhap nchini humo.
Shirika hilo la habari limenukuu
ujumbe kutoka kwa ikulu ya Urusi, Kremlin ingawa taarifa hio haijamtaja rasmi
Kim Jong-un.
Hata hivyo Yonhap linamnukuu afisa
mmoja wa wizara akisema kumtaja kiongozi huyo haina umuhimu wowote.
Kim Jong-un hajafanya ziara katika
nchi za kigeni tangu kuchukua mamlaka mwaka 2011.
Kituo chake cha kwanza kitaangaliwa
kwa karibu sana kwa sababu ya kile wnegi wanasema ni sera zake kanadmizi.
Mapema mwezi huu, taarifa zilisema
kwamba Urusi ndio itakuwa nchi ya kwanza kumwalika Rais Kim.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi,
Sergei Lavrov aliambia wandishi wa habari kuwa mnamo tarehe 21 mwezi Januari,
Rais Kim atapewa mwaliko wa kwenda Urusi kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa
vita vya pili vya dunia zitakazofanyika tarehe 9 mwezi Mei.
Hayati Kim Jong-il hakuzuru sana
nchi za kigeni, na wala haikutangazwa nchi alikonuia kwenda kabla ya siku ya
safari yake
Alisema kuwa dalili ya kwanza kutoka
kwa serikali ya Korea Kaskazini inaonyesha mambo yako shwari.
Shirika la habari la Yonhap lilisema
kuwa majibu wa taarifa kutoka kwa ofisi ya Rais wa Urusi, Rais wa Korea
Kaskazini ni mmoja wa viongozi walioalikwa kutoka nchi 20 na ambao
wamethibitisha kuhudhuria sherehe hizo.
Lakini barua hiyo haikuthibitisha
ikiwa Rais Kim ni mmoja wa walioalikwa wala ikiwa amekubali mwalikoi huo kwani
ilisema: ''Orodha ya watakaohudhuria haijakamilishwa, tunaendelea na mikakati
ya kuthibitisha wakaohudhuria.
Hapajakuwa na taarifa rasmi kutoka
kwa serikali ya Korea Kaskazini kuhusu tetesi hizo.
Kim Yong-nam, ambaye kikatiba ni
Rais asiye na mamlaka wa nchi hio ndiye amekuwa akiwakilisha Korea Kaskazini
katika mikutano katika nchi za kigeni.
Ziara za marehemu babake Rais Kim,
Kim Jong-il, hazikuwa zikitangazwa hadharani kabla ya yeye kuondoka nchini
humo.
No comments:
Post a Comment