Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amekanusha taarifa zilizoandikwa
kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini likiwemo gazeti la Mtanzania
kuwa amempeleka Diamond polisi kwa kile kinachosemwa ni kumtapeli
shilingi milioni 10.
Martin ameiambia Bongo5 kuwa Wema na Diamond hawadaiani chochote na kwamba habari hizo ni za uongo.
“Unajua tatizo ni kwamba hatujajua source ni nani,” amesema Martin. “Kwa
sababu taarifa ikishaingia kwenye social network everybody posts,
kwahiyo sisi tunamtafuta nani ameianzisha hiyo stori. “We don’t have any
issue with Diamond. Diamond hana issue yoyote na Wema,” amesisitiza.
“Kwahiyo tunashangaa ni kama ambavyo wanazusha sijui kafumwa na nani ni
uongo mtupu. Lakini nashangaa media ambazo zinaaminika zinaamua kuandika
story bila kumpigia simu mhusika au meneja na kuuliza ukweli wa hiyo
story.”
Kaazz kwel kwel ...
No comments:
Post a Comment