Thursday, 22 January 2015

KOMBE LA MATAIFA AFRICA CONGO YAWALAZA GABON 1 - 0


Tukiendelea kukuletea taarifa za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, yanayoendelea nchini Equatorial Guinea, jana usiku Congo iliweza kupata pointi tatu muhimu baada ya kuibwaga Gabon bao 1-0.
Katika mzunguko wa kwanza Congo ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Equatorial Guinea, huku Gabon ikiicharaza Burkina Faso mabao 2-0. Congo imepata ushindi wake wa kwanza katika michauno ya Kombe la Mataifa ya Afrika tangu fainali za mwaka 1974. Bao la Congo lilipatikana katika dakika ya 48 likifungwa na Oniangué. Congo ndiyo inayoongoza kundi A kwa kuwa na pointi 4 ikifuatiwa na Gabon yenye pointi 3, wenyeji Equatorial Guinea wakiwa katika nafasi ya tatu na pointi mbili. Mwisho ni Burkina Faso yenye pointi 1, baada ya jana kutoka sare ya kutofungana na wenyeji Equatorial Guinea katika mzunguko wa pili wa kundi A. Katika mchezo wa mapema wa kundi hili, Equatorial Guinea na Burkina Faso zimeshindwa kutambiana baada ya kukamilisha dakika 90 za mchezo zikiwa hazijafungana na hivyo kugawana pointi moja moja.


Sare yoyote na Burkina Faso Jumapili katika mzunguko wa tatu wa kundi A utaiwezesha Congo kufuzu kucheza hatua ya robo fainali. Kadhalika atakayeshinda kati ya Gabon na Equatorial Guinea katika mchezo wa Jumapili huko Bata, pia atafuzukuingia katika hatua ya timu nane yaani robo fainali.
Leo usiku ni mtifuano wa timu za kundi B, ambapo mchezo wa kwanza utazikutanisha Zambia na Tunisia na baadaye Cape Verde na DR Congo. Timu za kundi hili zote zina pointi moja moja.
Nayo timu ya Tanzania, Taifa Stars leo inakabiliana na majirani zao Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa katika mji wa Mwanza magharibi mwa Tanzania. Mwandishi wetu Shadrack Mwansasu ameandaa taarifa ifuatayo:
Na nchini Hispania Barcelona imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid katika michuano ya Copa del Rey hatua ya robo fainali. Bao la Barcelona limefungwa na Lionel Messi katika dakika ya 85. Timu hizi zitarudiana katika uwanja wa Atletico Madrid, Jumatano ya tarehe 28 mwezi huu

No comments:

Post a Comment