ARSENAL vs MONACO
Pamoja na kuibuka na ushindi wa
mabao 2-0 wakiwa ugenini katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo,
washika bunduki wa jiji la London Arsenal wameshindwa kusonga mbele
katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya
kwa kosa la kuruhusu magoli mengi wakiwa nyumbani katika mchezo wa
awali, ambapo Monaco iliwabamiza wenyeji wao hao Arsenal kwa jumla ya
mabao 3-1.
Kitimtimu hicho cha klabu bingwa Ulaya kilitimua vumbi pia huko nchini Hispania pale, Atletico Madrid ilipowakaribisha Bayer Leverkusen kutoka Ujerumani. Katika mchezo huo wenyeji Atletico wamefanikiwa kusonga mbele kwa mikwaju ya Penati baada kumaliza dakika 120 wakiwa mbele kwa bao moja ambalo halikutosha kuamua mshindi kutokana na matokeo ya mchezo wa awali ambapo Leverkusen iliibanjua .
Atletico bao moja kwa bila. Wakiwa mbele ya mashabiki wao lukuki Atletico ilishinda penati 3 dhidi ya 2 za wageni wao na kutinga moja kwa moja katika hatua ya robo fainali wakiungana na ndugu zao Real Madri.
Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa michezo miwili kupigwa. Borussia Dortmund watavaana na Juventus huku miamba ya soka ya Hispania Barcelona ikiialika Manchester City kutoka England.
No comments:
Post a Comment