Mwanamke wa Chechenya anayeishi
nchini Uholanzi amewachukua watoto wake wadogo kujiunga na wapiganaji wa
Islamic State nchini Syria kinyume na matakwa ya baba yao, wamesema
waendesha mashitaka nchini Uholanzi.
Baba mtalaka, Mholanzi, alivionya vyombo vya serikali kuwepo dhamira ya mtalaka wake na watoto kuondoka nchini humo.
Serikali inasema hili ni tukio la kwanza la aina yake.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye hakutambulishwa, amekuwa akiishi katika mji wa kusini mwa Uholanzi wa Maastricht.
Mwanamke huyo na watoto wake wawili hajaonekana tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana.
Wamefahamika kuwa walipanda ndege kutoka Ubelgiji kwenda Athens Ugiriki na mwanamke huyo anasemekana kuwasiliana na mama yake mwezi Januari, akisema wako katika mji wa Raqqa, nchini Syria, ngome ya wapiganaji wa Kiislam wa IS.
Waendesha mashita wanaichukulia kesi hiyo kama suala la utekeaji na wametoa hati ya kimataifa ya kuwakamata.
Lakini wanaeleza kuwa iwapo mwanamke huyo na watoto wake wamevuka mpaka na kuingia Syria, kuna uwezekano mdogo sana wa kuwarudisha nyumbani Uholanzi.
Raia wa Uholanzi wanaokadiriwa kufikia 200, baadhi yao wakiwemo wadogo, wanafahamika kujiunga na wapiganaji wa IS nchini Iraq na Syria.
No comments:
Post a Comment