Wednesday, 25 March 2015

EBOLA ILIUA IMEUA ASILIMIA % 90 YA WATOTO WADOGO WALIO UGUA

Picha ya Maktaba

Utafiti mpya umegundua kuwa Ebola, imesababisha athari mbaya zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima.

Asilimia 90 ya watoto chini ya mwaka mmoja ambao waliambukizwa walikufa.
Utafiti huo ulifanywa kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO na chuo kimoja cha London cha Imperial College London.

Utafiti umeonesha kwamba japokuwa kiwango cha watoto walioambukizwa ni kidogo kuliko watu wazima, watoto na watoto wachanga ambao walipata ugonjwa huo walikuwa na nafasi ndogo sana ya kupona.

Virusi hivyo vinavyosababisha homa kali na kutokwa damu ndani na nje ya mwili, vinaua asilimia 90 ya watoto wachanga katika mlipuko wa sasa.

Umeongeza kusemaa karibu asilimia 80 ya watoto wa umri kati ya mwaka mmoja na miaka mine hufa kama walivyogundua wanasayansi.

Zaidi ya watu elfu 23 waliambukizwa virusi vya ebola na zaidi ya elfu 10 walifariki dunia.

No comments:

Post a Comment