Tuesday, 31 March 2015

AJALI YA GERMAN AIRWINGS ... PICHA ZAIDI ZAPATIKANA ..

 NDEGE YA GERMAN AIRWINGS 

Gazeti moja nchini Ujerumani na jarida la Ufaransa yameripoti kuwa yameona picha za video zilizopigwa kwa simu zinazoonyesha dakika za mwisho ndani ya ndege ya Germanwings iliyoanguka katika milima ya Alps wiki iliyopita. Picha hizo za video zinadaiwa kuwa zilipatikana kwenye programu ya kuhifadhi kumbukumbu yaani memory-card iliyopatikana eneo la tukio.

 Katika picha hizo abiria ndani ya ndege hiyo wanaonekana wakipiga kelele huku sauti ya rubani na jitihada za kutaka kufungua mlango ili aingie kuokoa ndege hizo zikisikika. 

Rubani msaidizi wa ndege hiyo, Andreas Lubitz,anayeaminika kuwa ndiye aliyesababisha ajali hiyo alikuwa ndani ya chumba cha ndege huku akiqwa amefunga mlango mwenzake asiingie.

No comments:

Post a Comment