MAREHEMU SANI ABACHA RAIS WA ZAMANI WA NIGERIA ..
Serikali ya Switzerland inatarajiwa
kurejesha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 340 ambazo zilikuwa
zimeibwa wakati wa miaka ya 1990 wakati Rais Sani Abacha akiwa kiongozi
wa Nigeria.
Uswiss mwaka uliopita ilirejesha dola milioni mia saba kwa serikali ya Nigeria baada ya kumaliza mvutano wa kisheria.
Rushwa inabaki kuwa tatizo kubwa nchini Nigeria na katika mataifa ya nchi nyingi zinazoendelea hususan kutoka Afrika ambako wanasiasa mbalimbali wanatuhumiwa kujilimbikizia fedha katika mabenki ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment