Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.
Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo .Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.
David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege ,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini kilichotokea .
pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu,na hatua walizochukua kunusuru janga hilo.
Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea kurusha ndege? Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na nini walichokiacha na mambo kama hayo.
Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa taarifa ili tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea.
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Carsten Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Germanwings shirika dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea ajali hiyo kuwa isiyoeleweka.
niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika tasnia hii nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa,bado hainiingii akilini juu ya kile kilichotokea jana.
Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi kupoteza ndege yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama hayo ,bado hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali nzuri kiufundi na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia mafunzo ya hali ya juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa,kuhusika katika ajali mbaya kiasi kile .
No comments:
Post a Comment