Tuesday, 17 March 2015

JESHI LA NAIGERIA LASEMA HALINA TAARIFA ZA WASICHANA WALIOTEKWA ....>>


 Picha ikionyesha kijana akiwa na bango la kampeni ya kuwaokoa wasichana waliotekwa na Boko Haram. 

Jeshi la Nigeria, linalopambana kaskazini mashariki mwa nchi hiyo linasema halina habari yoyote mpaka sasa kuhusu wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram, miezi 11 iliyopita.

Shirika la habari la Ufaransa, AFP, linasema Luteji Jenerali, Kenneth Minimah, mkuu wa jeshi hilo alitoa ufafanuzi huo wakati akijibu swali la wanahabari waliotaka kujua hatma ya wasichana hao 219 waliopotea.

Minimah, akiongea katika mkutano wa baraza la usalama amesema katika maeneo yote waliyokomboa kutoka kwa wanamgambo hao pia waliwatafuta wasichana hao.

Amesema wanamgambo wa Boko Haram, wanapokimbia wanawachukuwa jamaa zao wote .
Ameongeza kusema  kwamba kila pale walipoulizia washichana hao wa Chibok, hakuna yeyote aliyetoa maoni yake kama aliona kuchukuliwa kwa washichana hao.

No comments:

Post a Comment