Kocha wa timu ya Taifa ya Malawi, Chimozi Yangi amesema Tanzania ina wachezaji wawili hatari na ndiyo waliowasumbua katika pambano hilo na kutamka wazi kuwa Mbwana Samata na Mrisho Ngassa ndiyo waliofanya pambano hilo kuwa gumu kwao haswa kipindi cha pili.
Malawi na Stars zilicheza juzi jijini hapa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na kutoka sare ya bao 1-1m huku bao la dakika ya 76 la Samata likifuta ndoto ya Malawi kuondoka na ushindi katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Yangi alisema waliwathibiti Stars haswa kipindi cha kwanza katika pambano hilo, lakini kuingia kwa Ngassa mambo yakawa magumu kwao kutokana na mchezaji huyo kuleta usumbufu langoni mwao, kitu kilichochangia kwa Stars kupata bao la kusawazisha.
Alisema japo mwanzo Samata peke yake alikuwaakiwasumbua lakini alipata upinzani kutoka kwa safu yake ya ulinzi jambo lililofanya ashindwe kufurukuta hadi alipoingia Ngassa.
“Huyu Samata na Ngassa kwa kweli walitupa kazi kubwa uwanjani japo mwanzo alipokuwepo Samata peke yaketuliweza kumthibiti, lakini alipoingia huyu mwenzake kazi ikawa kubwa ndiyo maana walipata bao la kusawazisha,” alisema Yangi.
Kwa upande wake, Samata alisema Malawi ni timu nzuri kutokana na kuwa na wachezaji wengi wa kulipwa na katika pambano hilo, nahodha Joseph Kamwendo anayekipiga naye TP Mazembe ndiye aliyewasumbua katika pambano hilo.
“Kamwendo tuko naye pale Mazembe, ametupa tabu sana leo katika hili pambano japo tuliweza kumthibiti asilete madhara makubwa,” alisema Samata.
No comments:
Post a Comment