Thursday, 19 March 2015

OBAMA AMPONGEZA NETANYAHU ...>>

Rais wa Marekani, Barack Obama.
RAIS BARACK OBAMA

Rais wa Marekani, Barack Obama, alimpigia simu kumpongeza waziri mkuu wa Irsael, Benjamin Netanyahu, Alhamisi, siku mbili baada ya kuchakguliwa tena kwa mhula wa nne.

White House inasema Bwana Obama, amesisitiza juu ya umuhimu ambao Marekani, unapatia ushirikiano wake wa kijeshi na usalama pamoja na Israel.

Kiongozi wa Marekani amerudia tena kueleza dhamira ya nchi yake ya kupatikana suluhisho la mataifa hayo mawili katika makubaliano yeyote ya amani kati ya Israel na wapalestina.
Mapema jana Bwana Netanyahu, alijaribu kukana kwamba haungi mkono suluhisho la mataifa mawili. 

Aliweza kuzusha wasiwasi wa kidiplomasia siku moja kabla ya uchaguzi wa bunge aliposema hakutakuwa na taifa la Palestina chini ya uongozi wake

No comments:

Post a Comment