Wajumbe wa mashirika ya kiraia wa vijiji vya Tama na Itala kusini mwa tarafa la Lubero jimboni kivu kaskazini, wanasema kutishiwa na kundi la waasi wa kihutu toka Rwanda wa FDLR kundi wanao ongozwa na Kanali Kizito.
Vitisho hivyo vinakuja kutoka uchapishaji wa ripoti wa mashirika ya kiraia katika sekta hio inayo bainisha hali ya harakati makundi ya waasi na wanamgambo katika maeneo hayo ambao wanahusika naunyanyasaji dhidi ya raia.Baadhi ya wanachama wa vyama vya kiraia katika vijiji vya Tama na Itala wanasema kua raia katika maeneo hayo wanaishi katika hali ya mafichoni kwa siku tano sasa kulingana na unyanyasaji kutoka waasi wanao hishi maeneo hayo hasa FDLR huku wakisema nawaishi kwa tabu wakilala usiku misituni.
Vitisho hivyo pia vinasababisha umati wa wakazi wamiji ya Kalevia, Bunyangenge, Bukumbirwa, Misingi, Mbwambali na Ikobo kuyaama makaazi yao nakuamia katika maeneo salama yanayo dhibitiwa na jeshi la taifa.
Mashirika ya kiraia wanaomba serekali kuanzisha operesheni zakijeshi dhidi ya waasi wa FDLR kuanzishwa pia kusini mwa Lubero ambako operesheni za kijeshi zimeanzishwa wiki chache dhidi ya waasi wakihutu toka Rwanda wa FDLR katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Baadhi ya vyanzo katika kanda hio zinaonyesha kuwa kiongozi wa waasi hao wa FDLR kanali Kizito wkundi maarufu la Foca,aliwateka nyara wanakijiji wa Mukeberwa na sehemu ya mji wa Kiyamba ilioko kusini mwa Tarafa la Lubero. Hata hviyo kiongozi huyo wa wanamgambo hao wa FDLR huwakataza wakaazi kuto toka ao kuingia ndani ya vijiji vyao.
Niwiki tatu sasa toka jeshi la hapa nchini FARDC kuanzisha harakati za kijeshi katika mkoa wa kivu kusini na kivu kaskazini ilikuwapokonya silaha waasi hao wakihuto kutoka rwanda wa FDLR ,harakati zinazoendeshwa mashambulizihayo na jeshi la Kongo peke yao baada ya serikali ya Congo kukataa msaada toka vikosi vya umoja wa matifa MONUSCO.
No comments:
Post a Comment